Miongoni mwa ratiba ya Atabatu Abbasiyya kuhusu wanafunzi wa vyuo vikuu: ni kuwatembeza katika miradi, kuwapa mihadhara ya kitamaduni na kuwapa uhuru wa kuuliza maswali mbalimbali.

Maoni katika picha
Mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel unaofanywa na idara ya mahusiano ya vyuo vikuu chini ya kitengo cha uhusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imekua na vipengele vingi vinavyo lenga mazingira ya vyuo ikiwa ni pamoja na kukaribisha wanafunzi, chini ya ratiba iliyo andaliwa na idara hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa vyuo na wala haiingiliani na muda wao wa masomo, inalenga kujenga maadili ya mwanafunzi wa chuo kwa kushirikiana na wakuu wa vyuo vyao na kuimarisha uwelewa na itikadi zao, sambamba na kuwatambulisha mafanikio yaliyopatikana katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kiongizi wa idara ya uhusiano ya vyuo vikuu Ustadh Azhar Rikabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Ukaribisho wa wanafunzi unafanyika kwa kuwasiliana na vyuo vikuu vya Iraq kupitia watumishi wa mradi, baada ya kuainisha idadi ya wanafunzi watakao karibishwa, Atabatu Abbasiyya huandaa gari za kuwabeba kutoka katika vyuo vyao hadi katika Ataba tukufu, wanapofika hufanya ziara kwa Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa pamoja, wakiongozwa na massayyid wanaofanya kazi katika Ataba hizo, baada ya hapo wanapewa maelezo kwa ufupi kuhusu miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Akaongeza kua: “Kwa kuwasiliana na kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya huteuliwa mmoja wa mashekh kwa ajili ya kutoa muhadhara wa kiitikadi na kitamaduni, unaoendana na kiwango cha wanafunzi na wenye kuwafaidisha katika maisha yao ya shuleni na nyumbani, mihadhara huendelea baada ya hapo na hubadilika na kua mihadhara ya kimaendeleo, hupewa mada zinazo zungumzia maendeleo ya kibinaadamu na huzungumzwa na wasomi walio bobea katika mambo hayo miongoni mwa watumishi wa Ataba tukufu, lengo ni kuwasaidia waweze kupambana na changamoto za kijamii na kitamaduni katika zama hizi za teknolojia, ukizingatia kua mwanafunzi wa chuo kikuu ni nguzo muhimu katika jamii”.

Akaendelea kusema kua: “Baada ya kumaliza kusikiliza mihadhara mbalimbali wanafunzi hutembezwa katika baadhi ya miradi inayotekelezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kama vile kiwanda cha Aljuud, chuo kikuu cha Al-Ameed, vitalu vya Alkafeel, hospitali ya Alkafeel, mashamba na mingineyo, ikiwa ni pamoja na taasisi ambazo zipo chini ya Ataba tukufu, na hupewa maelezo kuhusu miradi hiyo na umuhimu wake na kuwapa nafasi ya kuuliza maswali na kujadili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: