Kwa juhudi ya pekee inayofanywa na kitengo cha uhandisi cha askari namba 26 katika kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji ya kuweka uzio na handaki la ulinzi; kwa ajili ya kuimarisha usalama na kufanyia kazi maagizo ya makamanda wa kikosi cha Furat Ausat yaliyo tolewa katika upresheni ya pamoja, uzio huo umewekwa katika eneo la mpaka wa Karbala na Ambaar hadi katika wilaya ya Nukhaibu iliyopo katika mkoa wa Ambaar.
Viongozi wakasisitiza kua uzio huo unakusudia kulinda eneo la jangwa linalo weza kutumiwa na magaidi kufanya uharamia wao, baina ya jangwa na mji wa Najafu na Ramadi, pia uzio huo unalinda kwa kiasi kikubwa mkoa wa Ramadi kutokana na uharifu, urefu wa uzio umefika kilometa (120) kuanzia kiwanda cha saruji (Cement) hadi katika wilaya ya Nukhaibu kaskazini magharibi ya mkoa wa Karbala.
Yamesemwa hayo pembezoni mwa ziara ya makamo kiongozi mkuu wa opresheni ya Furat Ausatn kamanda wa kikosi Ali Hashimiy na mkuu wa kikosi namba/33 cha Furat Ausat Abdulhamiid Khaikani na mkuu wa kitengo namba 26/ katika kikosi cha Abbasi Maitham Zaidiy kwa ajili ya kukagua kazi ya uchimbaji wa handaki.
Wanao tekeleza mradi huu ni kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chini ya usimimiaji wa kikosi cha Furat Ausat. Viongozi wa kikosi cha Abbasi wamesema kua wanatarajia kumaliza kazi hii ndani ya mwezi ujao, wameomba wizara ya maji ishiriki katika kazi ili kukamilisha hatua ya pili inayo lenga kufikisha uzio hadi katika eneo la mpakani la Ur-ur.
Fahamu kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinalinda amani katika eneo la Karbala na Nakhibu kwa zaidi ya miaka minne, toka Daesh alipo vamia mkoa wa Ambaar, chini ya maelekezo ya viongozi wa Opresheni za pamoja.