Mazingira ya huzuni ya Fatwimiyya yatanda katika ardhi ya makao makuu ya maadhimisho ya Husseiniyya Karbala tukufu

Maoni katika picha
Ardhi ya Karbala tukufu mji mkuu wa maadhimisho ya Husseiniyya yametanda mazingira ya huzuni ya kuomboleza kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s), aliye fariki tarehe kumi na tatu Jamadal Uula –kwa mujibu wa riwaya ya pili- watu wa mji huu wamezowea kuadhimisha ziku za Fatwimiyya zinazo husu kumbukumbu ya kifo cha mbora wa wanawake wa duniani (a.s), jambo hili ni urithi wa watu wa Karbala, wamezowea kufanya maombolezo haya kila mwaka, mji umeenea mapambo meusi na barabara zimejaa mawakibu na vikundi vya husseiniyya kwa ajili ya kutoa huduma kwa mazuwaru wanaokuja kufanya ziara katika siku hizi za maombolezo, wamefunga mabanda yao kwa ajili ya kufanya majlisi za kuomboleza ambazo wanaonyesha majonzi na huzuni zao, hakika kumbukumbu hii inaumiza moyo wa kila muumini na mpenzi wa Ahlulbait (a.s), mazingira ya huzuni na kuomboleza yataendelea hadi siku ya kilele chake ambayo ni tarehe (13 Jamadal Uula) siku hiyo huitwa (Ashura ndogo).

Atabatu Abbasiyya tukufu haipo mbali na mazingira hayo, kama kawaida yake katika kuhuisha kumbukumbu za tarehe za vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), imeandaa ratiba maalum kwa ajili ya tukio hili, yenye vipengele vingi, ikiwemo program ya msimu wa huzuni za Faatwimiyya iliyo andaliwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya za Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu, itakayokua na matukio mbalimbali ya kuomboleza ikiwa ni pamoja na maonyesho ya vitabu, maigizo kuhusu dhulma alizo fanyiwa Zaharaa Batuli (a.s), pamoja na matembezi ya wanawake na ya watu wa Karbala kutoka pande zote za mji huu.

Kuhusu vipengele vingine vya maombolezo vitakavyo fanyika ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Abbasi, kutakua na mihadhara ya dini itakayo ratibiwa na kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya, watazungumzia utukufu wa bibi Zaharaa (a.s) na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, pamoja na kufanya majlisi ya kuomboleza msiba huo kwa watumishi wa Ataba tukufu ndani ya ukumbi wa utawala, pamoja na kualika wahadhiri na waimbaji wa kaswida na mashairi ya Husseiniyya watakao amsha hisia za huzuni katika msiba huu mkubwa uliowapata waislamu.

Kama kawaida yao katika kila msiba, watumishi wa Ataba mbili tukufu watafanya matembezi ya kuomboleza ya pamoja kwa ajili ya kuelekeza pole zao kwa Imamu wa zama Mahahi msubiriwa (a.f) kwa kifo cha bibi yake Zaharaa (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu imewekwa mapambo meusi na kuwekwa mabango yanayo ashiria huzuni katika kuta zake na korido zake pamoja na sehemu za nje, kama ishara ya kuingia msimu wa huzuni za Fatwimiyya, pia wataweka utaratibu wa uingiaji wa mawakibu ndani ya uwanja wa haram tukufu, maukibu hizo zitafanya matembezi kutokea katika eneo lao maalum ndani ya mji mkongwe wakipitia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kuomboleza msiba huu, kisha wanaelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, na kufanya majlisi ya matam ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: