Kwa mara ya kwanza nje ya Iran na ndani ya Iraq: Chuo kikuu cha Alkafeel chatoa mtihani wa lugha ya kifarsi.

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya lugha, kimetoa mtihani wa lugha ya kifarsi. Ukizingatia kua ndio mwakilishi pekee katika mikoa kumi na moja ya kati na kusini mwa Iraq, chini ya kituo cha kimataifa cha kufundisha lugha ya kifarsi katika chuo kikuu cha Fardusi mjini Mash-hadi, mwanafunzi anaefaulu katika mtihani huu anatunukiwa cheti cha lugha ya kifarsi kinacho muwezesha kujiunga na masomo kwenye chuo chochote nchini Iran, ambapo wamesoma kwa muda mfupi bila usumbufu wa kusafiri nje ya taifa kwa ajili ya kwenda kusoma lugha hiyo.

Mtihani umefanyika asubuhi ya Ijumaa (11 Jamadal Uula 1440h) sawa na (18 Januari 2019m), ndani ya ukumbi wa mitihani wa chuo kikuu cha Alkafeel kilichopo Najafu, jumla ya wanafunzi (28) wameshiriki katika mtihani huo kama sehemu ya maandalizi ya kujiunga na masomo ya sekula katika vyuo vya Iran.

Makamo rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Yahya Mahadi Almiyaliy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu mazingira ya mtihani huu: “Leo katika chuo kikuu cha Alkafeel tunatoa mtihani maalumu ya lugha ya kifarsi, kama mnavyo fahamu mitihani hii ni muhimu sana katika jamhuri ya kiislamu ya Iran, mtu yeyote anaetaka kujiunga na masomo katika vyuo vya Iran lazima afanye mtihani huu”.

Akaongeza kua: “Hakika mtihani huu unatokana na makubaliano yaliyo fanyika kati ya chuo kikuu cha Alkafeel na wizara ya elimu, maarifa na teknolojia ya Iran ambao unamuwezesha aliye faulu katika mtihani huu kujiunga na chuo kikuu chochote nchini Iran”.

Kiongozi wa idara ya lugha katika chuo kikuu cha Alkafeel Ustadh Mahmudu Faisal Swabbaar alisema kua: “Kwa mara ya kwanza hapa Iraq unafanyika mtihani wa lugha ya kifarsi chini ya makubaliano rasmi na chuo cha Fardusi kilichopo katika mji wa Mash-hadi, mtihani huu ni wa kiwango cha juu cha lugha ya kifarsi chini ya wizara ya elimu ya Iran, mtihani huu unafanyika sambamba na vituo vingine, na unatoa fursa kwa mwanafunzi kuweza kumalizia masomo yake nchini Iran, kwani sharti kubwa la kujiunga katika vyuo vya Iran ni kufaulu mtihani huu, unao tolewa na idara ya lugha hapa Iraq, kuna masomo mengine ya lugha ya kifarsi yanafundishwa miezi sita kukiwa na mitihani mitatu, pia mtu aliye soma masomo hayo anaweza kufanya mtihani huu”.

Kumbuka kua makubaliano ya kufundisha masomo haya, ambayo ni kiengereza na kifarsi, yanakusudia kuwarahisishia wanaohitaji kuendelea na masomo nje ya Iraq, tumesha fungua vituo vya kufundisha luhga za kigeni ambazo zi kiengereza na kifarsi zinazo muwezesha kujiunga katika vyuo vikuu vya kimataifa nje ya Iraq, tena kwa kusomea hapahapa Iraq bila kwenda nje na kwa garama nafuu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: