Marjaa Dini mkuu atuma misaada kwa wakimbizi waliopo katika mahema kwenye mkoa wa Swalahu Dini

Maoni katika picha
Bado mkono wa kheri na ubinaadamu wa kamati ya ustawi wa jamii chini ya ofisi ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani (d.dh), unaendelea kutoa misaada kwa wakimbizi wanao ishi katika mazingira magumu, safari hii wameelekea katika mkoa wa Swalahu Dini kwenye vituo vitatu, kituo cha kwanza kilikua katika wilaya ya Mu’taswim, na kituo cha pili katika hema za Shahaamah kwenye wilaya ya Tikrit, na kituo cha tatu ni kwenye majengo na maeneo yaliyo hamwa.

Rais wa kamati hiyo Sayyid Shahidi Mussawiy amesema kua: “Pamoja na ukubwa wa majukumu aliyo nayo Marjaa Dini mkuu lakini bado anayapa umuhimu mkubwa sana mambo ya kibinaadamu, hususan tatizo la wakimbizi, ametoa agizo kwa kamati ya ustawi wa jamii ambayo ipo chini ya ofisi ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani katika mji wa Najafu igawe vikapu (1500) vya aina mbalimbali za vyakula kwa wakimbizi ambao bado wapo katika mahema kwenye mkoa wa Swalahu Dini”.

Akabainisha kua: “Baada ya kumaliza kugawa chakula hicho wanufaika walitoa shukrani za dhati na wakasifu namna Marjaa anavyo wajali sawa na baba kwa wanae, wakawaomba wajumbe wa kamati ya ustawi wa jamii wawafikishie salamu zao na duo zao kwa Marjaa mtukufu.

Kumbuka kua kamati ya ustawi wa jamii inaendelea kutoa misaada mbalimbali kwa wakimbizi, kwa ajili ya kuwapunguzia matatizo walio nayo, na kuwajulisha kua Marjaa Dini mkuu ndio kimbilio sahihi la wairaq wote bila kujali rangi wala tabaka zao, na kuondoa picha mbaya inayo sambazwa na maadui.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: