Swidiqah Twahirah Fatuma Zaharaa (a.s) mbora wa wanawake wa duniani anauhusiano wa pekee na Qur’ani tukufu, yeye ndiye aliyeitwa: (Kitabu cha Mwenyezi Mungu kinacho tamka, Qur’ani ya kweli, Nuru ing’aayo, Mwanga uangazao, Mwenye mtazamo wa wazi, Siri zake ziko wazi, muonekano wake mtukufu, Muongozaji wafuasi wake katika radhi, kumsikiliza kwake hufikisha katika mafanikio, zinapatikana kwake hoja za Mwenyezi Mungu, malengo yake yako wazi, mwenye kujitenga na mambo ya haram, mwenye hoja za wazi, Utukufu wake umetukuka, ruhusa yake inapendeza na sheria zake zimeandikwa…).
Kutokana na uhusiano huo pamoja na kumuenzi tunahuisha kumbukumbu ya kifo chake, kituo cha miradi ya Qur’ani cha Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, kimeendesha kisomo cha Qur’ani ambacho hufanywa kila wiki kupitia mradi wa Arshu-Tilaawah ambao hufanywa jioni ya kila siku ya Ijumaa ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Hafla hii tukufu ya usomaji wa Qur’ani imehudhuriwa na watu wengi wapenzi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu na waombolezaji wa kifo cha bibi Zaharaa (a.s), wamenawilisha kubba na haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa visomo mwanana, wasomaji walikua ni; msomaji wa Atabatu Abbasiyya bwana Faisal Matwaru, na bwana Ahmadi Zamiliy mmoja wa wasomaji wa tawi la Maahadi katika mji wa Najafu, na bwana Sefu Himaam mmoja wa wasomaji wa mradi wa kiongozi wa wasomaji katika mji wa Najafu, mwisho akasoma kaswida mshairi Qassim Juburiy ambae aliikumbusha hadhira tukio la msiba wa Fatuma Zaharaa (a.s).
Kumbuka kua Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya inamiradi mingi ya Qur’ani tukufu, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Arshu-Tilaawah, unaolenga kunufaika na vipaji vya usomaji wa Qur’ani walivyo nao vijana wa Iraq na kuvifanya vionekane katika ulimwengu wa kiislamu, pamoja na kulea vipaji hivyo chini ya utaratibu maalum.