Bango kubwa linaloashiria msiba laonekana zaidi kushinda mabango mengine yaliyopo katika korido za haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imewekwa mapambo meusi na imejaa huzuni, inaonyesha wazi kuanza kwa msimu wa huzuni kwa watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika kumbukumbu ya kifo cha Mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s).

Mabango na vitambaa vinavyo ashiria msiba vimeenea katika korido zote za haram tukufu, kukiwa na kitambaa kikubwa kilicho wekwa juu ya mlango wa Kibla, kimedariziwa kwa uzi mweupe sentesi isemayo (Asalaamu Alaiki Ayyatuha Swidiiqah Shahiidah) na pembezoni mwa sentesi hiyo kumedariziwa maneno yasemayo (Yaa Faatwimah Zzaharaa), kitambaa hicho kilicho fika pande mbili za mlango wa kulia na kushoto kina urefu wa mita (28) na upana wa mita (6).

Mlango wa Imamu Hassan (a.s) unaotazama uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili nao umewekwa kitambaa kilicho dariziwa neno lisemalo: (Asalaamu Alaiki Ayyatuha Swidiiqah Shahiidah) kwa rangi nyekundu, likifuatiwa na neno lisemalo (Yaa Faatwimah Zzaharaa) na pembezoni mwake kuna maneno yasemayo (Rihaanat Nnabiy) kwa rangi ya kijani kama dalili ya bibi Zaharaa (a.s), kinaurefu wa mita (16) na upana wa mita (6).

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya maombolezo yenye vipengele vingi, kama vile; utowaji wa mihadhara ya kidini, kufanya majlis za kuomboleza, na imetangaza utayari wa kupokea mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya mji wa Karbala zinazo kuja kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: