Kwa macho yaliyojaa huzuni: Mawakibu za waombolezaji zinaingia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia idadi kubwa ya mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya Karbala mji wa mashahidi na undugu, wanaokuja kuomboleza kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s), sambamba na kujikumbusha mhanga mkubwa wa mbora wa wanawake wa ulimwenguni Fatuma Zaharaa (a.s) na kubainisha dhulma alizofanyiwa, na kuhimiza kushikamana na mwenendo wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), haya ndio mazowea ya waumini katika siku kama hizi zinazo umiza moyo wa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Harakazi za kuwasili mawakibu za waombolezaji katika msimu huu wa huzuni, unaoitwa (Muharam ndogo) zilianza kabla ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake, kilicho tokea mwezi kumi na tatu Jamadal Uula, siku hiyo ndio kilele cha maombolezo hadi usiku wake, humiminika katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, haya ndio mazowea ya uombolezaji tangu zamani.

Watumishi wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Huseiniyya wa Ataba zote mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) wameratibu matembezi ya mawakibu hizo, wanaingia kupitia mlango wa Kibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kumpa pole wanaelekea katika malalo ya muhusika mkuu wa msiba Imamu Abu Abdillahi Hussein (a.s), wakipitia katika uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu, makundi ya mazuwaru watukufu hushiriki pia katika matembezi hayo.

Kumbuka kua wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kote duniani wanaomboleza msiba huu wa kifo cha binti wa Mtume (s.a.w.w) bibi Fatuma Zaharaa (a.s), kuna riwaya tofauti kuhusu tarehe ya kifo chake na mahala lilipo kaburi lake (a.s), yote hayo yanaonyesha ukubwa wa dhulma alizo fanyiwa (a.s) hadi akamuhusia mume wake kiongozi wa waumini Ali (a.s), afiche eneo la kaburi lake na wala asihudhurie mazishi yake yeyote miongoni mwa waliodhulumu haki yake, alifariki akiwa na miaka kumi na nane kwa mujibu wa riwaya nyingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: