Sayyid Mussawiy aelezea hatua ya mwisho katika uhai wa bibi Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Sayyid Adnani Mussawiy kutoka kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu amezungumzia hatua za mwisho katika umri wa bibi mtasifu Fatuma Zaharaa (a.s), ambae hakuendelea kuishi baada ya baba yake (s.a.w.w) ispokua siku zilizo jaa huzuni na vilio akifanyiwa maudhi ya aina mbalimbali hakuna anaeyajua kwa undani ispokua Mwenyezi Mungu.

Hali kadhalika Sayyid Adnani Mussawi katika muhadhara wake alio zungumza kwenye majlis iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha bibi Fatuma (a.s) amezungumzia nyanja nyingi za maisha yake, akaelezea nafasi muhimu aliyokua nayo baada ya kifo cha baba yake (s.a.w.w), akasimulia namna alivyo dhulumiwa na mambo aliyo fanyiwa, akahusia wasikilizaji kunufaika na mafundisho yanayopatikana katika uhai wake na kuyafanyia kazi katika maisha yao ya kila siku, na umuhimu wa kufuata fikra za bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na kushikamana na mwenendo wake mtukufu, kwani yeye ndiye aliyekirimiwa na Mwenyezi Mungu mtukufu na akamfanya kua kiigizo chema na mbora wa wanawake wa duniani, akahimiza umuhimu wa kupambika na uchamungu na ikhilasi katika ibada, bibi Zaharaa (a.s) alikua zawadi kubwa sana ambayo Mwenyezi Mungu mtukufu alimpatia Mtume wake, na alikua mtu muhizi zaidi katika uhai wake (s.a.w.w), mpaka akasema: (Fatuma ni sehemu ya mwili wangu atakae mridhisha atakua ameniridhisha mimi na atakae muudhi atakua ameniudhi mimi).

Kumbuka kua wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wanaomboleza kifo cha mtoto wa Mtume (s.a.w.w) kila kona ya dunia, kuna riwaya tofauti kuhusu tarehe ya kifo chake na mahala lilipo kaburi lake (a.s), hii yote inaonyesha namna alivyo dhulumiwa hadi akamuhusia mume wake kiongozi wa waumini Ali (a.s) afiche sehemu ya kaburi lake, na asishuhudie jeneza lake yeyote miongoni mwa wale waliodhulumu haki yake, alifariki akiwa na miaka kumi na nane kwa mujibu wa riwaya mashuhuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: