Nani wa kumuosha Zahara … machozi yako yameingia kwenye maji
Ulihusia ukiwa na mbavu iliyovunjika … nani wa kuiosha na kuinyoosha
Ewe Haidari muache … unaona majeraha yanavyo msumbua
Wala usishike jeraha kwa mkono wako … ewe Haidari kila jeraha lina dawa
Tapaza sauti ya kuugulia ewe Karaar … muache hapo alipo muache
Beti hizi za kuomboleza ziliimbwa na mtumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kumpa pole Mtume mtukufu na wasii wake pamoja na wajukuu wake na Imamu Msubiriwa (a.s), watumishi wote wa myweshaji wenye kiu Karbala wanatoa mkono wa pole kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Swidiiqah Twaahirah Fatuma Zaharaa (a.s), kufuatia program ya kuomboleza iliyofanywa leo siku ya Jumatatu (14 Jamadal Uula 1440h) sawa na (21 Januari 2019m), katika siku hizi za msiba wa Fatwimiyya unao ombolezwa na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia ambao ni kumbukumbu ya kifo cha mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s).
Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wameimba kaswida zinazo huzunisha sana katika msiba huu wa Fatuma Zaharaa (a.s) macho yao yamejaa huzuni kubwa, walianza maombolezo hayo baada ya kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuimba wimbo wa Atabatu Abbasiyya wa (Lahnul Ibaa).