Kutokana na mafanikio yaliyo patikana katika mradi ulio anzishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu wa masomo ya masafa, kupitia Maahadi ya turathi za mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa wanaume, na chuo cha Ummul Banina (a.s) cha wanawake, kwa ajili ya kuboresha zaidi na kufanya masomo hayo yaendane na maendeleo ya kiteknolojia ya kisasa, tumeandaa darasa mjadala (nadwa) ya walimu wa taasisi mbili hizo za kielimu kwa ajili ya kujadili mazingira halisi ya ufundishaji wa kielektronik, na kutatua changamoto wanazo pata wanafunzi.
Kuhusu nadwa hii tumeongea na kiongozi wa Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) Shekh Hussein Turabi, amesema kua: “Uzowefu wa kusoma kwa mbali (elimu masafa) ni moja ya hatua nzuri zilizo patikana chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kulinda mafanikio haya, tumeandaa nadwa hii ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), kuna idadi kadhaa ya wanafunzi wa Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) walio shiriki katika nadwa hii na wanafunzi wa chuo cha Ummul Banina (a.s) cha wasichana pia wameshiriki, jumla kuna wanafunzi wakike na wakiume (100) kutoka katika mikoa ya (Bagdad, Karbala na Najafu) tutaalika wanafunzi kutoka mikoa mingine pia.
Akaongeza kua: “Tumejadili mambo mengi kuhusu mwalimu na mwanafunzi, tumeangalia changamoto mbalimbali na namna ya kuzitatua, sambamba na kupokea maoni mbalimbali yanayo lenga kuboresha masomo haya, vilevile kulikua na kipindi cha maswali na majibu, na tukapata maelezo ya vifaa vya kufundishia vinavyo tumiwa na Maahadi pamoja na chuo na namna ya kurahisisha ushirikiano wao pamoja na wanafunzi, sambamba na kushereheshewa namna ya kuendesha mitandao ya kielektonik ya toghuti zao”.
Akasisitiza kua: “Mwanafunzi anatakiwa kua mfuatiliaji wa elimu kwa faida yake na familia yake, bila kusahau umuhimu wa tabligh ya kielektronik na tabligh ya moja kwa moja katika ngazi ya familia na makazini kwa ajili ya kuendana na maendeleo za kisasa na kunufaika nayo”.