Watoto wa Zaharaa (a.s) miongoni mwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanaomboleza kifo chake…

Maoni katika picha
Katika kuhuisha kifo cha Swidiiqah Zaharaa (a.s) idara ya Masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya inafanya majlisi za kuomboleza msiba huu mkubwa zinazo fanyika kwa muda wa siku tano, tangu mwezi (13 Jamadal Uula) hadi mwezi (17).

Katika siku zote tano majlisi hizo zimekua zikihutubiwa na Sayyid Adnani Mussawiy kutoka kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, amekua akimzungumzia bibi Zaharaa (a.s) na dhulma alizo fanyiwa, pamoja na kuelezea utukufu wake mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume (s.a.w.w), sambamba na kusoma mashairi na kaswida zinazo amsha hisia za huzuni ya msiba huu unao umiza roho za wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Kiongozi wa idara ya Masayyid ambao ni watumishi Sayyid Mustwafa Dhiyaau Dini ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kila mwaka tunahuisha maumivu na huzuni zetu katika idara ya Masayyid ambao ni watumishi, watoto wa Zaharaa (a.s), kwa kufanya majlisi hii tukufu ambayo hudumu kwa muda wa siku tano, tulianza kufanya majlisi hii tangu miaka kumi iliyopita, na inaendelea kufanywa kila mwaka, hufunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha hufuatia muhadhara wa kidini”.

Akaongeza kua: “Majlisi huhitimishwa kwa matam ambayo husomwa na Sayyid Badri Mamitha mmoja wa watumishi wa idara ya Masayyid”.

Tunapenda kufahamisha kua Atabatu Abbasiyya tukufu inashuhudia uingiaji wa mawakibu za Husseiniyya zinazo kuja kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha Zaharaa (a.s), pia watumishi wa Ataba mbili walifanya matembezi ya kuomboleza msiba huu kwa pamoja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: