Uchoraji wa watoto wenye umri chini ya miaka kumi katika kongamano la msimu wa huzuni za Fatwimiyya awamu ya kumi na moja…

Maoni katika picha
Bibi Fatuma Zaharaa mbora wa wanawake wa ulimwenguni (a.s) anautukufu mkubwa katika nyoyo zetu sisi wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s), kwa nini asiwe na utukufu mkubwa wakati ni mtoto wa mbora wa walimwengu na Mtume wa mwisho, pia ni mke wa kiongozi wa waumini na mama wa Maimamu wawili Hassan na Hussein (a.s), kumpenda Batuli ni sawa na kuwapenda maimamu wote watakasifu, mapenzi yao yanapita katika miili yetu kama damu inavyo tembea ndani ya miili yetu, hatuwezi kuacha kumtaja na kutaja msiba wake, hali hiyo ipo hadi kwa watoto wetu, wanamtukuza na kumuenzi na kumfanya kua kiigizo chao katika uchamungu, taqwa, upole na elimu.

Kinacho fanyika katika kongamano la msimu wa huzuni za Fatwimiyya awamu ya kumi na moja linalo simamiwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya za Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, katika eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu katika kuomboleza kifo cha Batuli Zaharaa (a.s), kongamano hili linaonyesha wazi namna anavyo tukuzwa bibi huyu mtukufu, kielelezo kikubwa katika masomo ya watoto wetu ni namna wanavyo mpenda na wanavyo fuata mwenendo wate mtukufu, na namna wanavyo kumbuka dhulma alizo fanyiwa, kitengo tajwa hapo juu kimetenga muda kwa watoto wenye umri chini ya miaka kumi kwa ajili ya kuchora mitihani aliyopitia Swidiqah Twahirah (a.s) kwa kufuata vigezo vya fani ya uchoraji, katika kujikumbusha tukio la kuchomwa nyumba na kuvunjwa ubavu, katika eneo dogo la picha walilo andaliwa.

Tumeongea na rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyadhi Ni’mah amesema kua: “Kongamano la msimu wa huzuni la mwaka huu lilikua na kipengele maalum cha uchoraji kwa watoto wenye umri chini ya miaka kumi, walipangiwa kuchora masaaibu (matatizo) aliyopata Zaharaa (a.s), watoto hao wamepewa karatasi na rangi pamoja na kila wanacho hitaji katika uchoraji, na wakapewa nafasi ya kuhudhurisha (kukumbuka) tukio la kuchomwa nyumba na kuvunjwa ubavu, ili kila mmoja aweze kuchora picha ndogo kwenye karatasi yake yenye maana kubwa”.

Kuhusu lengo la kongamano hili amesema kua: “Lengo la kongamano hili ni kujenga mapenzi kwa Ahlulbait (a.s) kwa ujumla, na kwa namna ya pekee kwa bibi Zaharaa (a.s) katika nyoyo za watoto wetu, na kuujulisha ulimwengu kua kumpenda Mtume Mtukufu na watu wa nyumbani kwake watakasifu (a.s) ndio utambulisho wetu na ndio turathi yetu tunayo jivunia na kuirithisha kizazi baada ya kizazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: