Mbeba bendera ya Hussein (a.s) anabendera tatu ambazo hupandishwa kila mwezi katika kubba yake takatifu, hubadilishwa bendera kila baada ya siku kumi, uandaaji wa bendera hizo ni jukumu la idara ya ushonaji ya Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo ipo chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri cha Ataba.
Idara hiyo inamajukumu mengi, inawajibika kushona mapambo ya uwanja wa haram na mabango mbalimbali katika siku za matukio ya kidini na siku za kuzaliwa au kufariki kwa mtu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w).
Mtandao wa kimataifa Alkafeel umefanya mazungumzo na kiongozi wa idara hiyo Ustadh Abduzuhura Daud Selemani amesema kua: “Idara ya ushonaji inaofisi kuu mbili, ambazo ni: ofisi ya ushonaji na ofisi ya kudarizi, ofisi hizo hufanya kazi zote zinazo elekezwa katika idara ya ushonaji, kushona mabango, mashuka, mapazia na vinginevyo, kuhusu vitambaa ambavyo hufungwa ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Abbasi katika siku za matukio ya kidini asilimia kubwa huandaliwa kabla ya siku husika kwa muda wa siku hadi kumi, maandalizi yake hupitia hatua mbalimbali kama ifuatavyo:
Hatua ya kwanza: Vitambaa huandikwa na mwandishi mahiri Muhammad Husseiniy kutoka Maahadi ya Qur’ani ya Atabatu Abbasiyya kwa hati ya Thuluth, hutumia njia ya kielektronik ili kuwa rahisi kufanya baadhi ya marekebisho na kukuza maandishi au kuyapunguza kwa kutumia kompyuta.
Hatua ya pili: Maneno yaliyo andikwa huchapishwa kwenye karatasi maalum, kisha huletwa aina ya kitambaa kinachohitajika na kukiweka sehemu maalumu kisha hukatwa kwa kufuata herufi zilizo andikwa, baada ya hapo maneno hutenganishwa na kwenda kuyadarizi katika kitambaa ambacho mara nyingi huwa ni kitambaa cha thamani na chenye ubora mkubwa, mara nyingi huwa ni kitambaa cha (Qadifa) na mara nyingi nyuzi zinazo tumika ni za hariri”.
Akaendelea kusema kua: “Mwezi wa Muharam na Safar inaumaalum wake, huanza maandalizi ya vitambaa vitakavyo tumika katika miezi hiyo ya mwaka ujao mara tu baada ya kumaliza maombolezo ya miezi hiyo, sawa na kazi zingine ambazo huandaliwa mapema chini ya utaratibu ulio wekwa”.
Akaendelea kusema: “Bendera zinazo pandishwa katika kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) hutengenezwa chini ya utaratibu maalum, bendera moja hushonwa na kukamilika kwa muda wa siku mbili mfululizo, maandishi ya bendera nyekundu huandikwa na bwana Ahmadi Naaji, na maandashi ya bendera nyeusi ambayo hupandishwa katika mwezi wa Muharam huandikwa na Bwana Farasi Abbasi”.
Akasema kua: “Kutokana na ubaya wa hali ya hewa na aina ya matirio zinazo tumika kushona bendera za pande mbili hulazimika kubadilishwa bendera ya kubba tukufu la Abbasi (a.s) kila baada ya siku kumi”.
Akaendelea kusema kua: “Idara yetu hushona baadhi ya vitambaa vikubwa, kama bendera ya mgahawa wa nje wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo inaukubwa wa (mt16X13), pia kina kitambaa kikubwa kimewekwa mbele ya mlango wa Kibla na pembezoni mwake kwa nje, kitambaa kimoja kina upana wa mita (12) na urefu wa mita (6) na vimeandikwa maneno maalumu yanayo onyesha utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s), vitambaa vivyo huandaliwa na kushonwa na wataalamu wa idara ya ushonaji”.
Akamaliza kwa kusema kua: “Watumishi wa idara ya ushonaji ni mafundi waliobobea, wamefanya kazi miaka mingi na wanauzowefu mkubwa, kazi zote za ushonaji zinafanyika kwa kutumia mashine za kisasa ambazo zinatusaidia sana kuokoa muda, pia tunamiliki mashine za kudarizi kwa kutumia kompyuta, mashine hizo za kisasa zinauwezo wa kudarizi bango lenye ukubwa wa mita 3 kwa sentimita 60, hicho ni kiwango cha juu kabisa katika fani ya kudarizi, huwa tunaingiza vipimo katika kompyuta kisha tunaanza kudarizi kwa kutumia kompyuta”.