Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya imekizawadia chuo kikuu cha Tikrit zaidi ya vitabu (800) vya kielekronik, vitabu hivyo vinamasomo ya ngazi ya chuo pamoja na vitabu vya sheria mbalimbali, zikiwemo mada zilizo kusanywa kutoka katika majarida mbalimbali.
Jambo hili ni matokeo ya mafanikio makubwa ya kielimu yanayo enda sambamba na kubadilishana uzowefu na taasisi za kielimu, vitabu vyote vya kielektronik walivyo pewa kitovo cha haki katika chuo kikuu cha Tikrit vimetoka maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu na wamepewa bure.
Maktaba na Daru Makhtutaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu ipo tayali kuendelea kutoa kila wanacho hitaji miongoni mwa vitabu vya kielektronik, kwa ajili ya kusaidia wasomi na kuwapatia mahitaji yao katika safari ya kielimu.
Kumbuka kua maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya wanamiradi mingi inayo lenga kusaidia sekta ya elimu, hutoa zawadi ya nakala mbalimbali za vitabu wanavyo hitaji vya kielektronik na vya karatasi (kawaida), miongoni mwa misaada na miradi wanayo fanya ni kutunza matunda ya kielimu ya wairaq katika vyuo.