Shirika la usalama Alkafeel linaendelea kuwasaidia wananchi wa Iraq, na limejipanga kutopandisha pei za vocho (kadi za muda wa mawasiliano)

Maoni katika picha
Idara ya shirika la usalama Alkafeel (Mtandao wa familia ya kiiraq) katika harakati yake ya kusaidia raia wa Iraq na kupunguza tatizo la mawasiliano, imetangaza kutopandisha bei za vocha (kadi za muda wa mawasiliano) baada ya ongezeko la kodi la (%20), ili liendelee kua karibu na wananchi wa Iraq, idara ya utendaji chini ya maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya inajitahidi kuufanya kua ni mtandao wa wairaq wote.

Shirika la kiiraq linaona fahari kuwa na mtandao wa familia ya kiiraq unaowanufaisha wananchi wa Iraq –mia kwa mia unawanufaisha wafanya biashara na wafanya kazi- kupata ruhusa ya nne ya kumuhudumia raia watukufu wa Iraq, idara ya shirika la usalama Alkafeel imebainisha namna inavyo shikamana na maelekezo ya bunge la Iraq yanayo himiza kupunguza gharama za mawasiliano na huduma za Intanet ili kumuondoshea uzito mwananchi, na linajitahidi kutoa huduma kwa kila raia wa Iraq, linawahakikishia usalama wa mawasiliano yao kwa sababu linashirikiana na wizara ya mawasiliano na vitengo vyake vyote chini ya usimamizi wa wananchi wa Iraq.

Kumbuka kua mkuu wa kamati ya utendaji Ustadh Mhandisi Aarifu Bahashi amefafanua kua: “Hakika shirika linafanya kila liwezekanalo kuhakikisha linalinda huduma za mawasiliano ili kuwahudumia wateja wake waliojenga uwaminifu kwa shirika hili, na linafanya kazi kwa mujibu wa maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) na linahakikisha linabaki upande wa mwananchi katika kuhakikisha bei hazipandi pamoja na kuongezewa kodi mashirika ya mawasiliano likiwemo shirika letu”.

Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea toghuti ya shirika ifuatayo: http://alkafeelomnnea.com/contactus/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: