Kitengo cha Dini chatoa suluhisho la matatizo ya maisha ya ndoa kupitia machapisho yake

Maoni katika picha
Kutokana na juhudi zake katika kutafuta utatuzi wa matatizo yanayo enea katika jamii yetu, likiwepo tatizo la wanandoa na tatizo la ujane, kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya maelekezo ya kidini kimetoa vijitabu kwa jina la (Maelekezo ya ndoa).

Vijitabu hivyo vinalenga kumwongoza mwanaadamu maswala ya ndoa na kuhakikisha havunji sheria katika maisha ya ndoa, kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya maelekezo ya kidini ndani ya kitengo cha Dini Sayyid Muhammad Mussawiy, amesema kua: “Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu amemuumba mwanaadamu katika umbo bora zaidi, kwa ajili ya kuhakikisha anafuata njia ya ukamilifu na anafika katika radhi zake Mwenyezi Mungu mtukufu, lakini shetani na wafuasi wake wanaweza kuharibu safari ya mwanaadamu kwa kutumia matamanio yake”.

Akaongeza kua: “Hakika njia nzuri ya kumfanya mwanaadamu asiharibike ni kuoa, ni ngome imara inayoweza kumlinda na kumfanya ashinde vishawishi vya shetani”.

Kuhusu matatizo ya wanandoa akasema kua: “Hakika vijitabu vimebainisha sheria tulizo wekewa na Mwenyezi Mungu mtukufu ndani ya Qur’ani tukufu na zikafafanuliwa na sunna miongoni mwa hukumu muhimu, vijana wanaweza kuziona ziko juu ya uwezo wao au ngumu kuzifahamu”.

Akaendelea kusema: “Katika vijitabu hivyo tumebainisha matatizo ambayo huwapata zaidi wanandoa kwa njia nyepesi na rahisi kueleweka kwa vijana wetu ili kuwafanya waboreshe maisha yao ya ndoa”.

Ukitaka kuangalia (machapisho) vijitabu hivyo ingia katika toghuti ifuatayo: https://alkafeel.net/religious/index.php?iss
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: