Katika mfululizo wa ushiriki wake kwenye maonyesho na mahafali ya kitamaduni na kielimu, kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kimeshiriki katika maonyesho ya nane ya vitabu vya sheria yanayo simamiwa na muungano wa wanasheria wa Iraq kwa kushirikiana na chama cha mawakili cha mkoa wa Basra.
Ushiriki huu umetokana na mwaliko tuliopata kutoka kwa muungano wa wanasheria wa Iraq katika mkoa wa Basra, maonyesho yanafanyika ndani ya ukumbi wa Qasri Qadhaa katika mkoa wa Basra, maonyesho yamefana, kituo kimeshiriki kupitia tawi lenye kapu la machapisho tofauti ya aina mbalimbali, pamoja na machapisho maalum ya kituo, zikiwemo picha na nakala kale.
Ushiriki umekua na matokeo mazuri, kila aliyehudhuria na kutembelea tawi letu amesifu vitu vinavyo onyeshwa, pamoja na kupongeza kazi zote zinazo fanywa na kituo, wamesifu uamuzi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kuanzisha kituo hicho, na kazi mbalimbali zinazo fanywa na kituo hicho katika kuhuisha turathi za Basra, na kuondoa wingu la giza katika mkoa huo mtukufu.
Msemaji wa mahakama ya rufaa Hakim Jaasim Muhammad Mussawiy amesisitiza kua: “Maonyesho yanafanywa kwa mwaka wa nane, yanahusisha vitabu vya sheria na utamaduni, zinashiriki taasisi tofauti za usambazaji wa vitabu za ndani na nje ya Iraq, maonyesho yanakusudia kutambua vitabu vya mwisho kuandikwa katika sekta ya sheria pia ni fursa ya kubadilishana fikra”.