Nafasi na utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa Maimamu (a.s)

Maoni katika picha
Maimamu watakasifu (a.s) katika watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) kuanzia kwa Imamu Swadiq (a.s) hadi Imamu Mahdi (a.s), japokua hatujafikiwa na matamko yao ya moja kwa moja kuhusu Ammi yao Abulfadhil Abbasi (a.s), ispokua yaliyo tufikia kutoka kwa Imamu Haadi (a.s), yaliyo andikwa katika kitabu cha Iqbaal kwenye Ziyaatu Nnaahiyah iliyo pokewa kutoka kwake mwaka wa mia mbili hamsini na mbili hijiriyya, inayotaja majina ya mashahidi, katika ziara hiyo Imamu (a.s) anasema kumwambia Ammi yake Abbasi (a.s): ((Amani iwe juu ya Abulfadhil Abbasi mtoto wa kiongozi wa waumini, mliwazaji wa kaka yake kwa nafsi yake, aliyeitumia kesho yake katika jana yake, aliye jitolea kwake, ngao aliyekwenda na maji yake, aliye katwa mikono yake…)).

Na maneno ya Imamu wa zama (a.f) yaliyo tufikia kupitia ziara ya Nnaahiyah, ambayo anasema kua: ((Amani iwe juu ya viungo vilivyo katwa)).

Hakika Maimamu (a.s) wamekubaliana na yaliyo semwa na Imamu Swadiq (a.s) katika ziara ya Ammi yao Abulfadhil Abbasi (a.s), na waka amrisha wafuasi wao wamzuru (wasome ziara hiyo) ya Ammi yao Abbasi (a.s), kwa amri hiyo wanakua wamekubali heshima kubwa ya Abulfadhil Abbasi (a.s) iliyo tajwa katika ziara, hivyo tunaweza kusema: Hakika utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa Maimamu ambao hatujafikiwa na tamko lao la moja kwa moja kuhusu yeye ni uleule utukufu wake uliotajwa na Maimamu watakasifu (a.s), matamko yao yameungwa mkono na maimamu wengine kuhusu utukufu wake (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: