Huduma zinazo fanywa na watumishi masayyid kwa waombolezaji wa kifo cha bibi yao Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Mji wa shahada na uaminifu Karbala tukufu, unashuhudia misururu ya watu wanaokuja kutoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kumbukumbu ya kifo cha mbora wa wanawake wa ulimwenguni bibi Zaharaa (a.s), watu hao hupewa huduma na mawakibu za waombolezaji za Karbala, ni jambo la kawaida katika watoa huduma hao kuwakuta masayyid ambao ni watumishi wa malalo ya mwezi wa familia Abulfadhil Abbasi (a.s), wamekua na mawakibu ya kutoa huduma toka zamani, wanagawa chai kwa mazuwaru katika eneo la karibu na malalo tukufu.

Ugawaji wa chai katika siku za kuomboleza msiba wa Fatwimiyya ni kitendo cha urithi wa mababu na mababu kimekua kikifanywa na masayyid ambao ni watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kila mwaka masayyid hugawa chai kwa mazuwaru na waombolezaji wa kifo cha bibi yao Zaharaa (a.s) inayopikwa katika asili ya watu wa Karbala wa zamani.

Katika kudumisha utamaduni huo watumishi wengine pamoja na watu wa kujitolea nao hushiriki katika kugawa chai hiyo, tumeongea na kiongozi wa idara ya masayyid Sayyid Mustwafa Dhiyaau Dini amesema kua: “Karbala tukufu inaurithi muhimu wa kihistoria kuhusu uombolezaji wa vifo vya Ahlulbait (a.s), masayyid watumishi wameshikamana na urithi huo wa watu wa Karbala wa zamani”.

Akaongeza kua: “Kitu cha pekee katika maukibu hii ya kugawa chai ni namna chai hiyo inavyo pikwa kwa kufuata mapishi ya asili ya watu wa Karbala wa zamani, inapikwa kwa kutumia mkaa na inawekwa katika birika za zilizo kuwa zikitumiwa na watu wa kale (zamani), jambo hili humpa utulivu zaairu, na hutambua kua Karbala bado inaendelea kulinda turathi zake katika kuadhimisha matukio ya kidini”.

Akasema kua: “Maukibu hii ni urithi toka kwa mababu na mababu, inamamia ya miaka na hutoa huduma zake katika kuomboleza msiba wa Fatwimiyya, shughuli zake hufanyia sehemu maalumu ambayo ni jirani na uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hutoa huduma vilevile katika maombolezo mengine pamoja na mwezi wa Ramadhani”.

Kumbuka kua watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ambao ni masayyid wamejiunga chini ya idara inayo itwa (Idara ya masayyid watumishi), idara hiyo inamajukumu mengi, huongezeka majukumu yao katika vipindi vya ziara maalumu na tarehe za vifo vya maimamu wa Ahlulbait (a.s) kikiwemo kifo cha Zaharaa (a.s), wana utaratibu maalumu wa kuomboleza misiba hiyo, kwa kufanya majaalisi (vikao) vya kuomboleza au kushiriki katika maukibu za waombolezaji pamoja na kutoa huduma, mara utawakuta ndani ya haram tukufu, na mara utawakuta nje ya haram, wakiwa wamevalia nguo zao maalumu zinazo wapa nguzu za kiroho zaidi na kujenga utulivu kwa zaairu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: