Vipengele muhimu alivyo ongea Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Imamu Hussein leo (18 Jamadal Uula 1440h) sawa na (25 Januari 2019m) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), ameongolea vipengele vingi vya kimaadili na kimalezi, vinavyo endana na mazingira halisi tunayoishi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

 • - Yapasa kulinda sekta ya familia kutokana na mchango wake mkubwa katika kuharibu au kutengeneza jamii.
 • - Yatupasa kutambua kua chakula cha kiroho umuhimu wake haupungui kwa uchache wake tofauti na chakula cha kushikika.
 • - Malezi mema yamehimizwa na sheria na kusisitizwa na waja wema kuwa lazima familia zishikamane chini ya misingi na mienendo maalumu.
 • - Jukumu kubwa ni la baba wa familia.
 • - Kuna cheo na majukumu ya baba wa familia, akiyatekeleza yatamsaidia kua na familia salama.
 • - Mwalimu anajukumu kubwa katika kuandaa kizazi.
 • - Majukumu ya shule yanaihusisha familia na mwalimu.
 • - Jamii yetu inapitia wakati hatari sana.
 • - Mtu anapoona jamii yake, familia yake, watoto wake wanamatatizo, anatakiwa afanye juhudi ya kuyatutua na kila mmoja abebe jukumu lake.
 • - Baadhi ya muda mwanaadamu huwa na wajibu wa kuongea na kuhutubia, na kuna ambaye jukumu lake linakua ni kukubali, na kuna jukumu la wote.
 • - Heshima ya kijamii inamaanisha kua watu hukosana na kuelewana katika mambo fulani ambayo haitakiwi kuyakiuka, majukumu ya kijamii hasamehewi yeyote.
 • - Mazingira kwa ujumla tunakusudia uholela tunaoishi hivi sasa.
 • - Kuna tofauti kati ya mambo mawili haifai kuchanganya uhuru na uholela.
 • - Uhuru unahitaji nidhamu na kanuni na ndo zinazo linda uhuru.
 • - Uhuru hauna maana ya kufanya kila unacho taka.
 • - Hakuna maana kufanya kila unacho taka kwa kusingizia uhuru.
 • - Uhuru unakanuni zinazo bainisha kinachofaa na kisichofaa.
 • - Ukivunja haki za watu itatokea vurugu.
 • - Vurugu ni matokeo ya kukosekana utaratibu na kanuni.
 • - Lazima kuwe na kinga ya kijamii inayo zuwia kuvunja haki za watu.
 • - Jamii ikikosa kinga za kikanuni itaingia katika hatari kubwa ambayo haitaweza kutoka hadi kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
 • - Kinga za kijamii ni jukumu la kila mtu.
 • - Sisi ni jamii yenye misingi mizuri, utamaduni na mazowea tukichanganya mambo itakua vurugu.
 • - Yatupasa kukataa vurugu na uholela tuwe na uhuru wenye mipaka.
 • - Kunatofauti ya kufanya mambo kiholela kwa kusingizia uhuru na uhuru wenye kuheshimu kanuni na mipaka.
 • - Kuna mambo mengi yanafanyika kiholela yanatakiwa kurekebishwa.
 • - Tunatakiwa kurekebisha jamii na kuonyesha kua tunataka uhuru na sio vurugu.
 • - Hali itakua ngumu sana kama jengo la familia na jamii likibomoka.
 • - Lindeni jamii na misingi yake wala msiache mambo yafanyike kiholela.
 • - Msiwazoweshe watoto kufanya mambo kiholela wafundisheni uhuru wenye mipaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: