Kukamilika sehemu ya kwanza ya mradi wa uwekaji wa marumaru katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Utendaji mzuri wenye kutimiza viwango bora vya kiufundi kwa mujibu wa utaratibu ulio pangwa, sehemu ya kwanza ya uwekaji wa marumaru katika mradi wa kuweka marumaru kwenye haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika eneo lililopo baina ya mlango wa Imamu Ali Haadi (a.s) na mlango wa Furaat (Alqamiy).

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuhusu kazi hiyo: “Haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) tumeigawa katika sehemu kadhaa katika kuweka marumaru, ili kuepusha kusimama simama kwa kazi wanapo pita mazuwaru, kila sehemu tukimaliza kuweka marumaru tunaifungua na kuhamia katika sehemu nyingine, tutafanya hivyo hadi tumalize kuweka marumaru eneo lote la haram”.

Akaongeza kua: “Kazi inaendelea vizuri, tunatarajia kumaliza ndani ya muda uliopangwa pamoja na ugumu wa kazi, kazi hii inahusisha kuweka marumaru sehemu yote ya chini sambamba na kurekebisha mtandao wa umeme, maji taka, taa na mengineyo, pamoja na kazi zingine za maandalizi, kama vile kutoa marumaru za zamani na kusawazisha sakafu zinazo fanywa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi”.

Kuhusu wasifu wa marumaru amesema kua: “Marumaru ni za kawaida na adim (Malt Oksi), zina sifa nyingi, rangi zake ni za kawaida, zinauwezo mkubwa wa kuvumilia mabadiliko ya hali ya hewa, zina mwonekano mzuri, zinaupana wa (sm4) takriban”.

Kumbuka kua mradi wa kuweka marumaru katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), unachukuliwa kua ni mradi unaokamilisha miradi iliyo fanywa siku za nyuma, iliamriwa utekelezwe mradi huu kutokana na kuharibika kwa marumaru za zamani na kuharibika mwonekano kutokana na ukongwe wake, kwani zina zaidi ya miaka (50), uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya uliona umuhimu wa kufanyika kwa mradi huu kwa ajili ya kuongeza uzuri wa sehemu miongoni mwa sehemu za peponi, ili kuweka muonekano mzuri utakao ingiza furaha katika nafsi ya zaairu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: