Kituo cha kupiga picha nakala kale cha Atabatu Abbasiyya, miongoni mwa wageni walio kitembelea ni ujumbe wa idara ya kupiga picha nakala kale (makhtutwaat) kutoka Atabatu Alawiyya takatifu, kwa ajili ya kuangalia ufundi na vifaa vya kisasa zaidi vinavyo tumika katika fani hiyo, sambamba na kuimarisha mazingira ya kufanya kazi kwa kushirikiana, kwa ajili ya kulinda turathi za kiislamu kwa ujumla na kwa namna ya pekee kulinda turathi za Maimamu wa Ahlulbait (a.s) kielimu na kivitendo katika kufikia lengo hilo.
Mkuu wa kituo cha nakala kale (makhtutwaat) cha Atabatu Abbasiyya Ustadh Swalahu Siraji ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Ziara hii ni miongoni mwa ziara nyingi zinazo pokelewa na ofisi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, zinazo lenga kubadilishana uzowefu na kuimarisha ushirikiano wa kimaktaba kati ya maktaba za Ataba tukufu na maktaba za Iraq kwa ujumla”.
Akaongeza kua: “Ugeni uliokuja umetembelea korido za kituo na umeangalia mitambo inayo tumika pamoja na hazina ya nakala kale na picha, wameonyesha kufurahishwa na umakini wa kazi na mafanikio yaliyo fikiwa pamoja na njia za kisasa zinazo tumika katika upigaji picha wa nakala kale na faharasi”.
Kiongozi wa wageni ameelezea lengo la ziara yao kua ni kunufaika na uzowefu wa watumishi wa kituo cha kupiga picha nakala kale na faharasi kilicho chini ya maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ukizingatia kua ni kituo chenye jina kubwa na mafanikio makubwa yanayo shuhudiwa na kila mtaalamu wa mambo ya upigaji picha wa nakala kale na faharasi, awe wa ndani au nje ya taifa.
Mwisho wa ziara wakafanya makubaliano ya ushirikiano wa kitamaduni na kielimu baina ya pande mbili kwa maslahi mapana ya kutunza nakala kale na turathi za Iraq, kisha ugeni ukapewa zawadi za machapisho ya kituo, picha na nakala kale za Atabatu Abbasiyya tukufu.