Kituo cha uzalishaji Alkafeel chapata tuzo tatu katika shindano la kimataifa la Aafaani.

Maoni katika picha
Kituo cha uzalishaji Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia wapiga picha wake mahiri Saamir Husseini na Haidari Munkushi wamepata tuzo tatu za juu katika shindano la kimataifa la Aafaani la picha za mnato, lililofanyika Saudia na kuratibiwa na nchi za kiarabu chini ya usimamizi wa shirikisho la kimataifa la wapiga picha na Jumuwiya ya wakiga picha ya Marekani, pamoja na taasisi kadhaa za kimataifa.

Jumla ya wapiga picha (1709) kutoka nchi (122) wameshiriki katika shindano hilo, mpiga picha wetu Saamir Husseini amepata nasafi ya kwanza katika kipengele cha Portrait, naye mpiga picha Haidari Mankushi akapata nafasi ya pili katika kipengele hicho hicho na Wasaam Sharafu akashinda katika kipengele cha mwanzo (sifuri).

Kushiriki mashindano haya na kupata tuzo ni sehemu ya mwendelezo wa tuzo walizo pata wapiga picha wa Atabatu Abbasiyya tukufu, za kitaifa na kimataifa, kutokana na uwezo wa hali ya juu walio nao pamoja na msaada wanaopewa na viongozi wao, chini ya Atabatu Abbasiyya inayo fanya kila iwezalo katika kuendeleza wataalamu wake.

Rais wa shindano la kimataifa Aafaani Majdiy Nasri Aalinasri amesifu ushiriki wa wairaq katika shindano hilo, akasema: “Kazi za wairaq zilizo shiriki katika shindano hili zilikua na ubora wa hali ya juu, hakuna iliyokua mbaya”.

Akaongeza kua: “Maranyingi kazi za wairaq huwavutia watawala, kwa sababu kazi zao kuwa nzuri zenye ujumbe unao eleweka, hazihitajii kufikiri sana ili uweze kujua maana ya picha”.

Tunapenda kuwajulisha kuwa hii ni mara ya pili kushiriki katika shindano la kimataifa la Aafaani ambalo hufanywa katika nchi ya Saudia, wameshiriki wapiga picha kutoka kutoka kila sehemu ya dunia wakiwa na picha za aina tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: