Barabara ya kitamaduni ya Zuberi imejaa bidhaa za kielimu na kitamaduni za Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Miongoni mwa barabara za kitamaduni ambazo zimeenea katika miji mingi ya Iraq, ni ile iliyopo kwenye wilaya ya Zeberi katika mkoa wa Basra, barabara hiyo imesheheni mamia ya machapisho ya vitabu tofauti vya lugha, falsafa, Dini na elimu za kisekula, na kua moja ya sehemu muhimu za kitamaduni katika wilaya hiyo, Atabatu Abbasiyya tukufu haikubaki nyuma katika kuonyesha machapisho yake ya vitabu.

Barabara ya kitamaduni ya Zuberi hupangwa bidhaa Jumamosi ya kila wiki, watu wenye maktaba walipenda miongoni mwa vitabu vinavyo onyeshwa viwemo vinavyo chapishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, hilo lifanyike kwa kushirikiana na kitengo cha habari na utamaduni ili kuwafanya wawe washiriki wa kudumu katika maonyesho ya wilaya ya Zuberi, wameshiriki kwa kuonyesha hazina ya vitabu tofauti na majarida yanayo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kuonyesha picha za mnato zilizo pigwa kwa ustadi na utaalamu wa hali ya juu.

Kila aliyetembelea maonyesho hayo amesifu na kufurahishwa na machapisho yaliyo onyeshwa, kwani yanaendana na mapenzi yao pia hayalengi sekta moja, yanalenga sekta tofauti na yanatumia njia nzuri na nyepesi kueleweka katika kufafanua mada tena kwa viwango tofauti.

Tunatarajia kuona barabara hii katika siku zijazo inakua na ongezoko kubwa la watu watakao tembelea maonyesho haya miongoni mwa vijana wanaosoma katika mji wa Basra hususan watu wa wilaya ya Zuberi, kwa kushirikiana na maktaba pamoja na vituo vya usambazaji wa vitabu vilivyopo katika wilaya ya Zuberi kwa ajili ya kuja kuonyesha machapisho yao mbalimbali katika barabara hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: