Wito wa kushiriki watafiti wa kike katika program ya kongamano la kielimu la wanawake

Miongoni mwa picha za kongamano
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni Rabiu Shahada awamu ya kumi na tano litakalo fanyika mwezi wa Shabani ujao chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hussein (a.s) ni mnara wa umma na mrekebishaji wa maadili), imetoa wito kwa wahadhiri wa kike wajitokeze kushiriki kongamano la kielimu la wanawake lenye anuani isemayo: (Mwanamke baada ya Ashura: utafiti katika kuangalia changamoto za sasa) litakalo fanyika katika kongamano la wanawake. Kamati imeteua mada zifuatazo:

Kwanza: mada za kifikra na kimaarifa:

  • 1- Aina ya jamii (jinsia) utafiti kuhusu mwingiliano wa nafasi ya mwanamke na nafasi ya mwanaume kwa kuangakia yaliyotokea katika vita ya Twafu.
  • 2- Nafasi ya mwanamke katika kupambana na fikra potofu kwa kuwaiga wanawake waliokuwepo katika vita ya Twafu.
  • 3- Utafiti wa utunzi wa wanawake kuhusu tukio la Husseiniyya (vitabu, barua, maoni, tafiti na makala).
  • 4- Athari ya kielimu ya mwanamke katika kufanikisha mahafali za kimataifa kuhusu swala la Husseiniyya.
  • 5- Marjaiyya wanavyo mzungumzia mwanamke na athari yake katika kujenga jamii (mifano kutoka katika watu walioshiriki kwenye vita ya Twafu).
  • 6- Athari za uwelewa wa wanawake katika vita ya Twafu.

Pili: mada za kijamii na maendeleo endelevu:

  • 1- Nafasi ya mwanamke katika kulinda amani kwenye jamii kwa mujibu wa mafundisho kutoka katika vita ya Twafu.
  • 2- Nafasi ya mwanamke katika kumjenga kiongozi mwenye mafanikio.
  • 3- Mwanamke baina ya kunyanyaswa katika familia na jamii.
  • 4- Nafasi ya mwanamke katika kuleta mabadiliko na maelewano.
  • 5- Athari ya utamaduni katika kujenga familia.

Tatu: mada za kuhusu haki na sheria:

  • 1- Uhuru wa mwanamke kati ya sheria za kiislamu na mazowea ya kikabila.
  • 2- Utekaji wa wanawake kati ya sheria za kiislamu na kanuni za kimataifa.
  • 3- Namna ya kupambana na matatizo ya kivita kwa kuangalia msimamo wa wanawake waliokuwepo katika vita ya Twafu.
  • 4- Sheria ya kuhudhuria wanawake katika uwanja wa vita, (utafiti wa yaliyo fanyika katika vita ya Twafu).

Kuhusu masharti ya ushiriki ni:

  • 1- Utafiti usiwe umeshawahi kuandikwa au kusambazwa na watu wengine.
  • 2- Uandikwe kwa kufuata vigezo vya kielimu.
  • 3- Usiwe chini ya kurasa (15) na usizidi kurasa (25) za A4.
  • 4- Uandikwe kwa hati ya (Simplified Arabic), herufi ziwe na ukubwa wa saizi (14) na hamishi saizi (12) na utunzwe kwenye (CD).
  • 5- Maneno yasizidi (300) na uambatanishwe na muhtasari wake.
  • 6- Uwekwe ukurasa wa majina ya vitabu rejea mwishoni mwa utafiti huo.
  • 7- Utafiti utokane na mada tulizo taja.
  • 8- Kamati ya maandalizi haitapokea utafiti ambao hautakamilisha masharti yaliyo wekwa.
  • 9- Tafiti zitumwe pamoja na muhtasari wake na wasifu (cv) ya mwandishi na namba yake ya simu katika anuani hii ya barua pepe: tansiq@warithanbia.com kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu zifuatazo: (07735380747 - 07813053831).

Kuhusu muda kamati imebainisha kua: Mwisho wa kupokea tafiti hizo ni (1 /3 /2019m) tafiti zitakazo kubaliwa kushiriki zitatangazwa tarehe (9/ 3/ 2019m), watapewa maelezo kamili kuhusu kongamano (siku ya kongamano – sehemu na ratiba ya kongamano) kabla ya (1/ 4/ 2019m).

Kumbuka kua kongamano linalenga kuangazia mwenendo wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) namna walivyo kua wakimchukulia mwanamke, katika vita ya Twafu na matukio mengine yaliyo fuatia, na namna ya kubadilisha mwenendo huo na kuufanyia kazi katika zama zetu sambamba na kuangalia maswala ya mwanamke kwa ujumla, na kuonyesha nafasi yake katika uislamu, na kusahihisha fikra potofu zinazo sambazwa kuhusu mwanamke, kwa sababu tatizo sio uislamu bali ni mabaki ya kifikra na historia iliyo mnyima mwanamke haki yake aliyopewa na uislamu, pamoja na kuangalia changamoto anazo kutana nazo leo mwanamke kwa kulinganisha na vita ya Twafu, na namna ya kutatua changamoto hizo baada ya kuzitambua, pamoja na kuonyesha uwezo wa elimu ya mwanamke na athari yake katika kupambana na changamoto, kwa kumpa nafasi ya kielimu kwa ajili ya kuzifanyia utafiti changamoto hizo kwa kufuata vigezo vya kielimu na kuja na ufumbuzi wa kinadharia na kivitendo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: