Toleo la tatu katika mfululizo wa (Manaraat) anaona nuru…

Maoni katika picha
Hivi karibuni katika kitengo cha ujumbe na maoni ya chuo chini ya kituo cha (Al-Ameed Duwaliyyu Lilbuhuthi wa Dirasaat) cha Atabatu Abbasiyya tukufu limetoka toleo la tatu katika mfululizo wa Manaraat, vinavyo toka kwa anuani ya: (Michango ya kifikra ya wanachuoni wa kishia na watafiti wake katika jarida la Uislamu wa Kairo 1949 / 1972 somo la kihistoria) la Alaa Muhsin Swadiq A’araji baada ya toleo la kwanza na la pili, toleo hili ni sehemu ya kukamilisha yaliyomo katika matoleo ya kwanza pia ni sehemu ya kujiandaa na matoleo yajayo.

Tumeongea na Dokta Alaa Kaadhim Muslawi rais wa kitengo cha ujumbe na maoni ya kituo cha Al-Ameed amesema kua: “Kituo cha Al-Ameed kinafuraha kuwaletea wasomaji wake watukufu toleo la tatu la mfululizo wa matoleo ya (Manaraat), ambalo limejikita katika kubainisha michango ya kifikra ya wanachuoni wa madhehebu ya Imamiya na Maraajii wake pamoja na watafiti wa jambo muhimu, nalo ni kujenga ukaribu baina ya madhehebu, lengo kubwa la mradi huu ni kuweka ukaribu mitazamo ya madhehebu za kiislamu, na kuelezea itikani ya madhehebu ya shia ili kuondoa chuki kwa baadhi ya wanachuoni wa kiislamu kutokana na shaka walizo nazo dhidi ya shia katika baadhi ya mambo na kujenga ukaribu wa wazi, na kuondoa wasiwasi katika ufahamu wao na kujitenga na matamanio binafsi ya baadhi ya watu”.

Akaongeza kua: “Jambo hili limekuja sambamba na haja ya umma wa kiislamu ya kutambua maoni ya wanachuoni wa kishia na watafiti wake katika sekta ya kijamii, kifiqhi na zingine, makala iliyo andikwa katika jarida la (ujumbe wa kiislamu la Kairo) imekua na matokeo makubwa kwa wanadini na wanachuoni wa umma, sawa iwe ndani ya mada zilizo andikwa, au katika msimamo wa hoja na ubainifu, ilikua na bado iko hivyo msimamo wa wanachuoni ni kufuata mwenendo sahihi wa kutegemea Qur’ani na sunna tukufu pamoja na hadithi za Ahlulbait (a.s), na kulingania undugu na kujitenga na ikhtilafu na malumbano baina ya madhehebu, mwenendo huo ndio njia pekee ya kulingania Dini ya Mwenyezi Mungu na ujumbe wa Mtume wake mtukufu (s.a.w.w)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: