Kamati ya maelekezo na misaada yakitembelea kikosi cha Swalahu Dini na yawabebea zawadi wapiganaji…

Maoni katika picha
Bado kamati ya maelekezo na misaada chini ya kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kusaidia wapiganaji wa Hashdi Sha’abi wa vikosi mbalimbali, chini ya utaratibu maalum uliopangwa, utaratibu huo unahusisha asilimia kubwa ya vikosi vilivyopo katika uwanja wa vita, sawa sawa uwe wakati wa mapambano au baada ya mapambano, leo kamati hiyo imetia nanga katika mkoa wa Swalahu Didi, kuwapatia walicho nacho kutoka katika mkono wa kheri na utowaji, kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi hii wanaifanya chini ya kauli mbiu isemayo (Kuwatumikia ndio fahari yetu).

Rais wa kamati Shekh Haidari Aaridhwi ametuambia kuhusu msafara huo kua: “Kazi yetu ya kutoa misaada ya kimaana na kimkakati bado inaendelea, tuna ratiba ya kutembelea vikosi vingi, safari hii ni moja kati ya misafara mingi tuliyo nayo, sasa hivi tunatembelea mkoa wa Swalahu Dini katika miji ya Spaikar, Aujah na Sajlah, tumefurahi kukutana na walinda amani wa miji hiyo, nayo ni miongoni mwa miji ambayo hushuhudia uvunjifu wa amani kutoka kwa magaidi, tumewafikishia salamu na dua kutoka kwa Marjaa Dini mkuu, na amewasisitizia umuhimu wa kushikamana na usia wake wa kuwa makini na kuchukua tahadhari ya vitimbi vya magaidi wa Daesh, vile vile tumewafikishia salamu na dua za ndugu zao watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kuwapa vitu na zawadi ya tabaruku kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Aridhwi akabainisha kua: “Kamati ilikutana pia na wakazi wa mji wa Sajlah na vitongoji vya jirani yake, na kuwahusia washirikiane na wanajeshi na kudumisha undugu na mawasiliano kati yao”.

Wapiganaji wametoa shuktani zao kwa Marjaa Dini mkuu kutokana na misaada anayo wapatia kwa kuwatumia ujumbe mbalimbali kupitia Ataba tukufu, wakabainisha kua msaada wa Marjaa kwao unawapa moyo na kuwatia nguvu ya kuendelea kujitolea katika kulinda taifa dhidi ya maadui wa Iraq na ubinaadamu, wameapa kuendelea kuwa wapiganaji waaminifu kwa taifa lao, ukizingatia kua Iraq ni taifa lenye maeneo matukufu, taifa la mawalii na waja wema, wamesema kua: “Tunamuahidi Mwenyezi Mungu kuwa tutaendelea kua panga kali mkononi mwa Marjaa mtukufu”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu hutuma misafara ya kutoa misaada ya chakula na vifaa kwa wapiganaji wa vikosi vyote vya Hashdi Sha’abi na vya serikali, pamoja na kuunda kamati maalumu kwa ajili ya kusaidia familia za mashahidi na kufuatilia hali za majeruhi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: