Mwezi ishirini na mbili Jamadal Uula ni kumbukumbu ya kifo cha Qassim (a.s)...

Maoni katika picha
Mwezi ishirini na mbili Jamadal Uula wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) huwa katika majonzi na maombolezo, ni siku aliyo fariki mtu mwenye karama nyingi Qassim mtoto wa Imamu Mussa bun Jafari Kaadhim (a.s) katika mwaka wa (192h).

Kuhama kwake katika mji wa babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w):

Imamu Qassim (a.s) alihama katika mji wa babu yake (s.a.w.w) na kuelekea Iraq pamoja na msafara wa wafanya biashara ili kujificha na njama za maadui waliokua wakiwaandama na kumtesa Imamu Kaadhim (a.s), kutokana na kuwa kwao mwendelezo wa nyumba ya Mtume na ndio chemchem ya hekima na elimu na ndio rehma kwa waumini, walipata manyanyaso ya aina mbalimbali, ikawa sababu ya watoto wa Imamu Kaadhim (a.s) kusambaa sehemu tofauti duniani, kwa ajili ya kumlinda Imamu Ridhwa (a.s) pamoja na Qassim (a.s) aliyekua anajulikana kwa elimu yake na ukubwa wa upeo wa akili yake na uchamungu wake.

Sifa zake:

Alikua (a.s) anaheshima kubwa mjukuu mwerevu miongoni mwa wajukuu wa Mtume (s.a.w.w), ndugu mtakatifu miongoni mwa nduzu wa Imamu, alikua mtu wa pekee katika ulinganiaji wake na uchamungu wake na mitihani aliyo pata baada ya ndugu yake Imamu Ridhwa (a.s), yatosha katika kuelezea utukufu wake yale yaliyo pokewa na Thiqatu Islamu Shekh Kulaeini (q.s) katika kitabu cha Usulul Kaafi: kutoka kwa Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s) kutoka kwa Yazidi bun Salitwi kutoka kwa Imamu Kaadhim (a.s) walipokua katika njia ya Maka Imamu alimwambia: (...Nakuambia ewe Abu Ammaarah mimi nimetoka nyumbani kwangu nimemuhusia mwanangu Fulani na nikamshirikisha na mwanangu kwa uwazi na nikamuhusia kwa siri, nikamwambia peke yake laukama amri ingekua kwangu ningeujalia (Uimamu) kwa mwanangu Qassim kutokana na ninavyo mpenda, lakini ni amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu anamteua amtakae).

kifo chake:

alifariki Qassim (a.s) baada ya maradhi makali aliyo ugua mwaka wa (192h) katika ardhi ya Suriy kwenye mtaa wa Bakhamra, sehemu lilipo kaburi lake hadi sasa likiwa na kubba ya dhahabu na minara mikubwa ikitoa nuru ya utukufu na ukarimu unaoshuhudiwa na watu wa mbali na wakaribu na kusifiwa na kila mtu, watu wamemuweka katika mimbari ya ufahari ya ndani ya moyo.

usia wake:

miongoni mwa usia wake (a.s) kwa ammi yake Shekh Hayyi aliye owa mmoja wa bindi zake alimwambia: (Ewe Ammi.. Nikifa niosho na univishe sanda na kunizika, ukifika msimu wa hijja nenda kahiji pamoja na binti yako na binti wangu huyu, ukimaliza ibada ya Hijja nendeni Madina, mtakapo fika katika lango la mji wa Madina mtangulize binti yangu, wewe na mke wangu mtembee nyuma yake, hadi mtakapofika katika mlango mrefu hiyo ndio nyumba yetu, ataingia katika nyumba hiyo humo atakuta wanawake tu na wote ni wajane).

Utekelezaji wa usia:

Mwaka wa pili baada ya kufa Qassim (a.s) Shekh Hayyi alikwenda kuhiji, akafuatana na mtoto wa Qassim, ikawa kama alivyo sema Qassim, binti wake alikwenda moja kwa moja hadi katika mlango akagonga na akafunguliwa, wakina mama wa bani Hashim wakamzunguka, wakamuuliza jina lake na hali ya baba yake, mama yake Qassim alipotoka na akamwangalia akaanza kuita: Ewe mwanangu Ewe Qassim.. wallahi huyu ni yatima wa Qassim. Kisha binti akawaambia kua babu yake na mama yake wamesimama mlangoni, inasemekana kua mama yake Qassim baada ya kufahamu yaliyo mkuta mwanae aliugua na hakuendelea kuishi ispokua siku tatu na akafa.

Fadhila za kumzuru (a.s):

Sayyid ibun Twausi katika kitabu chake cha Misbaahu Zaairu katika fadhila za ziara yake (a.s) ameunganisha na ziara ya Abulfadhil Abbasi mtoto wa kiongozi wa waumini na Ali Akbaru mtoto wa Imamu Hussein (a.s), alisema: (Ziara za waja wema na watoto wa Maimamu (a.s), ukitaka kumzuru mmoja wao kama vile Qassim mtoto wa Kaadhim na Abbasi mtoto wa kiongozi wa waumini na Ali bun Hussein aliye uwawa katika vita ya Twafu (a.s) na wengine ambao wako sawa na wao, utasimama katika kaburi lao..., kuna hadithi iliyo sikika kutoka kwa Imamu Ridhwa (a.s) kua alisema: (Asiye weza kunizuru mimi basi amzuru ndugu yangu Qassim).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: