Kufanyika kwa shindano la (Ibswaar) upigaji picha za mnato kwa wanawake…

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na tano ya mwaka (1440h /2019m) imetangaza kufanyika kwa shindano la kupiga picha za mnato kwa wanawake.

Wanaopenda kushiriki waangalie masharti ya shindano na watume picha zao za ushiriku kwa utaratibu ulio pangwa, miongoni mwa masharti ni:

  • 1- Picha zitumwe kwa (JPG) na kwa umakini mkubwa.
  • 2- Mshiriki awe na umri wa miaka (17) na zaidi.
  • 3- Hairuhusiwi kuongeza kitu katika picha kama vile (tarehe, sahihi na vinginevyo).
  • 4- Idara ya mashindano inahaki ya kutumia picha katika jambo lolote la kiuchapaji.
  • 5- Picha isiwe imesha shiriki katika shindano lingine au imesha tumiwa na chombo kingine cha habari.
  • 6- Unaweza kushiriki kwa bicha mbili na sio zaidi.
  • 7- Mwisho wa kupokea picha zitakazo shindanishwa ni (10/ 3/ 2019m).

Kamati imeandaa zawadi zifuatazo kwa washindi:

Mshindi wa kwanza: (500,000) dinari laki tano za Iraq.

Mshindi wa pili: (400.000) dinari laki nne za Iraq.

Mshindi wa tatu: (300,000) dinari laki tatu za Iraq.

Picha zitumwe kwenye barua pepe ifuatayo: Women.media89@gmail.com na kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu zifuatazo: (07435000578 / 07804738704).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: