Kwa ushiriki zaidi ya wahadhiri (300) wakike na wakiume: idara wa wanawake yafanya semina ya kuwajengea uwezo…

Maoni katika picha
Kwa lengo la kujenga uwezo wa wahadhiri wa mimbari ya Husseiniyya na kuwafanya waendane na ukubwa wa ujumbe wanaotakiwa kuufikisha, idara ya wahadhiri wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeratibu semina ambayo inawashiriki zaidi ya (300) wanaume na wanawake.

Semina itachukua siku kumi, kwa kukaa saa mbili darasani kila siku, inafanyiwa ndani ya sardabu ya Imamu Ali Haadi (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya ukufunzi wa mwalimu wa uhadhiri na mkuu wa Maahadi ya Imamaini Alhasanaini (a.s) ya uhadhiri katika mji mtukufu wa Qum Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Muhsin Hakiim.

Kuhusu semina hii tumeongea na Sayyid Ali Khatibu msaidizi wa mkuu wa Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) ya wahadhiri wanaume katika Atabatu Abbasiyya tukufu aliye alikwa rasmi na idara ya wahadhiri wa kike na amesema: “Hakika mhadhiri wa kiume na wakike wa mimbari ya Husseiniyya ana nafasi kubwa na yenye athari katika jamii na kidini, kimaadili na kifikra, wanaeneza uwelewa wa kiislamu kutokana na wanayo zungumza, hivyo kuandaa semina za aina hii kuna umuhimu mkubwa katika kuboresha uwasilishaji wa khutuba na kuzifanya ziendane na mazingira yetu ya sasa, semina hii imekuwa na mwitikio mkubwa kutoka kwa wahadhiri wenye uzowefu mkubwa”.

Naye makamo kiongozi wa idara ya wahadhiri wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadhat Taghriid Abdulkhaaliq Tamimi amesema kua: “Idara ya wahadhiri wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu inalipa umuhimu mkubwa sana swala la kuwasilisha ujumbe katika mimbari, daima inajitahidi kuboresha na kuongeza uwezo wa wahadhiri, ndio sababu ya kuandaa semina hii ya kuwajengea uwezo wahadhiri wote wa mimbari ya Husseiniyya, ili kuhakikisha tunaboresha kiwango cha mhadhiri na kumfanya aendane na maendeleo ya sasa katika uzungumzaji wake na njia za uwasilishaji, na mengineyo yanayo changia kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe wa Imamu Hussein (a.s) kwa tabaka zote za wanajamii pamoja na kutofautiana viwango vyao”.

Kuhusu mada za semina amesema kua: “Semina ina mada nyingi, zote linalenga kutengeneza njia nzuri ya kufikisha utamaduni wa Husseiniyya katika jamii kwa namna inayo endana na umuhimu wa kufikisha ujumbe katika zama zetu, pamoja na kufafanua ukubwa na jukumu walilonalo wahadhiri katika kupambana vita vya kifikra na kiitikadi vinavyo elekezwa katika dini ya kiislamu kila wakati, hali kadhalika mkufunzi ameelezea umuhimu wa kushikamana na misingi ya lugha ya kiarabu, na kutumia rejea za uhakika wakati wa kuzungumza kwenye mimbari, mada nyingine ilikua inahusu umuhimu wa wahadhiri kuchagua maneno mazuri yenye athari nzuri wakazi wa kuzungumza, na utaalamu wa kutumia muda vizuri na kuto refusha mada, na kugawa fikra ndani ya muda muwafaka, pamoja na kuchagua mada na kuzungumza bila chuki (taasubu), sambamba na namna ya kubadilisha sauti wakazi wa kutoa khutuba”.

Kumbuka kua lengo la kuanzishwa idara hii ni kusaidia kujenga uwezo wa wahadhiri wa kike kutokana na umuhimu mkubwa walio nao hususan kipindi cha maombolezo, kuwatoa pembezoni na kuwafanya waweze kusaidia kufikisha ujumbe wa kudumu wa Husseiniyya kwa njia bora zinazo eleweka na halisia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: