Kutokana na mafanikio makubwa: Hospitali ya rufaa Alkafeel yafanya upasuaji zaidi ya elfu (16) ndani ya mwaka 2018m…

Maoni katika picha
Mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Muhammad Azizi ametangaza kua; hospitali imefanya upasuaji (16,866) ambao ni upasuaji wa kujeruhi na mionzi ndani ya mwaka 2018m, kiwango cha mafanikio kilikua ni kikubwa kilikaribia (%90) hicho ni kiwango kikubwa kwa mujibu wa viwango vya kitabibu vya kimataifa.

Akaongeza kua: “Hakika upasuaji wa mwaka jana umezidi idada ya upasuaji uliofanyika mwaka juzi, kwa idadi na kwa aina pia, ni upasuaji wa aina zote, mkubwa, wa kati na mdogo, asilimia kubwa upasuaji ulikua unafanywa na madaktari wa kiiraq wenye uwezo mkubwa unao endana na vifaa tiba vilivyopo katika hospitali na wakaweza kuleta mafanikio haya”.

Kuhusu shughuli za upasuaji Azizi amesema kua: “Hakika hospitali imefanya idadi kubwa ya upasuaji, miongoni mwake ni upasuaji maalumu upatao (571), upasuaji juu ya mkubwa upatao (2841), upasuaji mkubwa upatao (3619), upasuaji wa kati upatao (1390) na upasuaji mdogo upatao (658).

Akaendelea kusema: “Upasuaji ulihusisha upasuaji wa majeraha upatao (869), upasuaji wa kupandikiza viini upatao (736), upasuaji wa moyo wazi upatao (127), upasuaji wa macho upatao (1638), upasuaji wa kutumia mionzi upatao (2157), upasuaji wa kuvunjika mifupa upatao (931), upasuaji wa wanawake upatao (2207), upasuaji wa kubadili chembechembe hai upatao (171) na upasuaji wa njia ya mkojo upatao (341)”.

Mkuu wa idara ya hospitali Ustadh Muhammad Haadi ameongeza kua: “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu yamesaidia kutoa huduma za kijamii kwa mamia ya wagonjwa, tena katika mikoa tofauti ya Iraq, huduma hizo zilihusisha kutibu wagonjwa au kuwafanyia upasuaji bila malipo”.

Kuhusu mahusiano, kiongozi wa idara ya habari na uhusiano Ustadh Hassan Hussein Aaridhwi amesema kua: “Hakika hospitali hufanya shughuli za kibinaadamu na kimatibabu za aina mbalimbali mbele ya vyombo vya habari vya kitaifa kwa gharama nafuu za matibabu au hufanya upasuaji kwa bei ya punguzo wa watu wenye kipato kidogo na mafakiri”.

Katika wilaya ya Hindiyya hospitali ya Alkafeel ilifunga hema na kuendesha program ya (BMVSS) Aaridhwi amesema kua: “Kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa tulifanikiwa kugawa viungo bandia zaidi ya (600) kwa majeruhi wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi pamoja na walio shambuliwa na magaidi, sambamba na wale waliopoteza viungo vyao kwa maradhi mbalimbali”.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel unaweza kutembelea toghuti ya hospitali: www.kh.iq au piga simu: (07602344444 / 07602329999).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: