Benki ya walimu na nafasi yake katika kufikia malengo ya kimalezi

Maoni katika picha
Katika kuhakikisha malengo ya kimalezi yanafikiwa, idara ya elimu chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea kufanya warsha za kujenga uwezo kwa walimu wenye shahada za juu.

Siku ya Jumatamo (23 Jamadal Uula 1440h) sawa na (30 Januari 2019m) imefanya warsha ya kujenga uwezo chini ya anuani isemayo: (Malengo ya kimalezi ni miongoni mwa vipaombele muhimu kwa wataamumu bobezi).

Mkufunzi wa warsha ya leo Muhammad Ma’amuri amesema kua: “Mafunzo yanahusu kujenga uwezo kwa watumishi walio jiunga hivi karibuni katika kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu wenye shahada za juu, wanajengewa uwezo katika eneo la kuunda swali zuri lenye athari linalo endana na malengo ya malezi yaliyo wekwa katika selebasi ya masomo kusudiwa”.

Akabainisha kua: “Maudhui za warsha hii zinalenga kujenga uwelewa kuhusu malengo ya malezi kwa makundi kusudiwa yenye mafungamano ya moja kwa moja na namna halisi ya kumjenga mwanaadamu, pamoja na misingi ya kielimu kusudiwa, kupitia warsha hii tunatarajia kutengeneza kizazi kitakacho jitenga na malengo hasi (mabaya), kitakuwa kizazi kizuri chenye elimu kinacho fanya mambo mazuri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: