Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, chatumia kitengo chake cha wahandisi kupambana na athari za mvua hapa njini

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinatumia wahandisi wake kupambana na changamoto yeyote inayo weza kusababishwa na mvua hapa mchini, hususan maeneo ambayo huwa na mvua nyingi na miji ya magharibi ambayo hushuhudia maporomoko makubwa ya maji kutoka Sirya na Jodan.

Uongozi wa kikosi umeongea na vyombo vya habari na kusema kua: “kitengo cha wahandisi kipo tayali kushughulikia tatozo lolote linaloweza kutokea kwa sababu ya mvua kwa kushirikiana na viongozi wa jeshi la muungano na serikali ya eneo husika, wahandisi wako tayali kutoa misaada ya kitaalamu na kutoa mahitaji ya lazima”.

Akasema kua: “Wametumwa wawakilishi kadhaa katika mikoa kuandaa mabomba ya ziada na mitaro mikubwa itakayo saitia kupitisha maji ya maporomoko”. Akasisitiza kua maandalizi hayo yanafanyika sambamba na kulinda uharibifu wa mazingira baada ya kuwamaliza magaidi wa Daesh, kikosi kinafanya kazi za ujenzi na kutoa misaada ya kibinaadamu katika sekta mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: