Kituo cha faharasi na kupangilia ma’alumaat chafanya semina kwa watumishi wa maktaba ya kitivo cha adabu ambacho kipo chini ya chuo kikuu cha Bagdad

Maoni katika picha
Kituo cha faharasi na kupangilia ma’alumaat chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa mafunzo ya faharasi za kisasa na namna ya kutumia program ya (Kuha) kwa watumishi wa maktaba ya kitivo cha Adabu – katika chuo kikuu cha Bagdad yaliyo dumu siku tano, yalianza Jumapili (27 Januari) hadi Alkhamisi (31 Januari 2019m).

Mkufunzi wa semina hiyo iliyo kua na mada mbalimbali alikua ni kiongozi msaidizi wa kituo cha faharasi na kupangilia ma’alumaat Ustadh Saamir Baasim, amesema kua: “Semina hii inalenga kujenga uwezo wa kimaktaba kwa watumishi wa maktaba”.

Akaongeza kua: “Washiriki wameelekezwa namna ya kutumia program ya kisasa inayo tumika kwa kiasi kikubwa katika sekta ya maktaba duniani”.

Kumbuka kua semina hii imefanywa kutokana na maombi kutoka kwa kitivo cha adabu chini ya chuo kikuu cha Bagdad, maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu inamichango mingi na miradi mbalimbali inayo lenga kuongeza elimu za watafiti, kwa kuwapa wanacho hitaji miongoni mwa vitabu na machapisho ya kielimu na maarifa ya yasiyo shikika na yanayo shikika (Soft copy na hard copy), miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa kuhifadhi matokeo ya kielimu ya wairaq katika ngazi ya chuo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: