Namna ya kunufaika na likizo yako kupitia Qur’ani…

Maoni katika picha
Kwa lengo la kunufaika na likizo kupitia Qur’ani na kuongeza uwezo wa kuisoma, kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Maahadi ya Qur’ani tukufu ya Atabatu Abbasiyya, kimetangaza kuanza usajili wa wanafunzi watakao shiriki semina za mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomaji wa Qur’ani hapa Iraq katika kipindi cha likizo. Kituo kimebainisha kua: Usajili utafanyika kuanzia tarehe 5 – 10 Februari 2019m, na mlango wa kushiriki katika semina hii uko wazi kwa wasomaji wote wa hapa Iraq, kutakua na mtihani wa jaribio tarehe (10/2/2019) watakao faulu katika mtihani huo watapelekwa katika semina itakayo fanyika (11 – 16/2/2019).

Kituo kimeweka masharti ya kushiriki katika semina kama yafuatayo:

  • 1- Mshiriki awe na umri wa miaka (18 – 35).
  • 2- Awe anajua hukumu za Tajwidi (usomaji) na awe anajua aina za sauti.
  • 3- Mtihani wa majaribio utafanyika kupitia video ya usomaji wa mshiriki, isiwe imerekodiwa nyuma ya tarehe (28/1/2019).
  • 4- Mshiriki anatakiwa kutaja majina yake matatu, mkoa anaotoka na jina la taasisi ambayo yuko chini yake na tarehe ya kuzaliwa kwake pamoja na kutuma picha yake.
  • 5- Taasisi itaweka video za washiriki katika ukurasa maalum wa Facebook ya (kituo cha miradi ya Qur’ani) kuna mambo yapasa yazingatiwe wakati wa kurekodi.

Njia na masharti ya kurekodi video:

  • 1- Uwe usomaji wa tajwidi unao eleweka na usiokua na makosa.
  • 2- Picha isiwekwe vitu vingine vya ziada wala sauti isiongezewe vionjo.
  • 3- Picha iwe ya kisasa na irekodiwe rasmi kwa ajili ya kuingia katika semina hii.
  • 4- Video isizidi dakika sita.
  • 5- Kamera isiwe mbali na msomaji.
  • 6- Anatakiwa awe amevaa vizuri wakati wa kujirekodi.
  • 7- Viteo zitumwe kwenye telegram kupitia namba hii (07827740369).
  • 8- Kila mshiriki atume video moja tu, hairuhusiwi kutuma zaidi ya moja au kubadilisha, atakae fanya hivyo hataruhusiwa kushiriki.
  • 9- Sehemu inayo takiwa kusomwa kwenye jaribio ni katika surat Ahzaab (kuanzia aya ya 38/ Maakaana alaa Nnabii…) hadi (aya ya 48/ Wakafaa billahi wakiilaa).

Kuhusu vigezo watakavyo tumia kamati ya majaji ni:

  • - Kuangalia hukumu za usomaji (tajwidi, kusimama na kuanza).
  • - Mpangilio wa sauti katika usomaji.
  • - Naghma katika usomaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: