Atabatu Askariyya tukufu inajiandaa kuweka makumbusho yake maalumu, na makumbusho ya Alkafeel imeonyesha utayali wa kusaidia hilo

Maoni katika picha
Makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeonyesha utayali wake katika kusaidia kuanzishwa kwa makumbusho maalum ya Atabatu Askariyya tukufu.

Wamesema hayo baada ya kupata mwaliko wa Atabatu Askariyya, ambapo ujumbe wa makumbusho ya Alkafeel umekwenda kutembelea malalo ya Maimamu wawili Askariyyain (a.s), na ukakutana na viongozi wa Atabatu Askariyya tukufu akiwemo katibu mkuu Mheshimiwa Shekh Sataar Murshidi, ugeni ulisikiliza malengo ya mradi huo pamoja na kutembelea sehemu iliyo teuliwa kuwekwa makumbusho hiyo.

Rais wa kitengo cha makumbusho ya Alkafeel Ustadh Swaadiq Laazim amesema kua: “Kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Ataba zetu tukufu, na kutokana na uzowefu wa makumbusho ya Alkafeel katika mambo ya kimakumbusho, tumetembelea Atabatu Askariyya tukufu kwa ajili ya kuchangia uwekaji wa mikakati ya awali katika kuweka makumbusho itakayo kua sehemu ya hazina za turathi za malalo hiyo tukufu”.

Akaongeza kua: “Tumeangalia sehemu inayo tarajiwa kuwekwa makumbusho, ambayo patakua na ukumbi wa maonyesho na stoo, tutafanya kazi kwa pamoja kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu katika kuanzisha jambo hili takatifu”.

Katibu mkuu wa Atabatu Askariyya tukufu Mheshimiwa Shekh Sataar Murshidi amezungumzia umuhimu mkubwa walionao Atabatu Abbasiyya katika kusaidia Ataba zingine ikiwemo Atabatu Askariyya tukufu, akasema: “Hakika lengo letu ni kuanzisha makumbusho rasmi ya Atabatu Askariyya tukufu, kwa ajili ya kuonyesha vifaa vya kimakumbusho vilivyopo katika Ataba kwa ujumla na mabaki ya madhara yaliyo fanywa na shambulizi la kigaidi katika haram tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: