Vipengele muhimu alivyo ongea Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa ya leo (25 Jamadal Uula 1440h) sawa na (1 Januari 2019m) iliyo swaliwa ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai (d.i) amezungumzia vipengele muhimu vya kimaadili na kimalezi vinavyo endana na mazingira halisi tunayo ishi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

 • - Miongoni mwa majukumu yetu ya msingi ni kubainisha mafundisho ya Mwenyezi Mungu.
 • - Miongoni mwa majukumu yetu ya msingi ni kuijulisha jamii mambo yanayo tishia kuvunja misingi ya kimaadili na kuvunja amani na kuilinda jamii na mambo hayo.
 • - Miongoni mwa mambo yanayo tishia ustawi wa jamii ni kuenea kwa uzushi na kutangazwa habari za uongo.
 • - Kuna wakati ulimi hutumika vizuri na wakati mwingine hutumika vibaya.
 • - Kalamu ni sawa na ulimi wa pili na yaweza kua na madhara makubwa zaidi ya ulimi.
 • - Haiwezekani jamii yeyote kufikia malengo yake bila kuwa na maelewano na mshikamano.
 • - Bila kuaminiana hamuwezi kufikia malengo mnayo tarajia.
 • - Ulimi au kalamu vikiwa vikweli na viaminifu vinaweza kua msingi wa kheri na maelewano katika jamii.
 • - Ulimi au kalamu vikisambaza uongo na uzushi vitakua ni msingi wa kueneza shari katika jamii.
 • - Uzushi na uongo yamekua mambo ya kawaida katika jamii hii ni hatari mno kwa ustawi wa jamii.
 • - Miongoni mwa baadhi ya mambo yanayo wafanya watu wazushe na kusema uongo ni husda.
 • - Tamaa ya madaraka na mali husababisha mtu aseme uongo au azue uzushi ilia pate anacho kitaka.
 • - Kuna watu wengi wanajifanya ni watu wa dini na wanaandika uongo na uzushi mwingi katika mitandao ya kijamii.
 • - Kufanya haraka kuamini vitu bila uchunguzi hupelekea kusaidia kusambaza uongo na uzushi kwa wanachuoni wa dini na waja wema.
 • - Kutuhumu watu hasa wanachuoni wa dini na watu wema ni miongoni mwa madhambi makubwa na kosa baya sana.
 • - Kumzushia uongo msomi wa dini hupelekea watu wajitenge nae na wasinufaike na elimu yake.
 • - Baya zaidi ni pale tunapo saidia kutangaza uongo bila kujua.
 • - Muumini akitaka kuongea hukaa kimya kidogo kisha anayaongea maneno hayo katika moyo wake yakiwa na kheri anayasema na kama yana shari anayaacha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: