Miongoni mwa mikakati ya kuongeza kiwango cha utendaji wa wanawake katika jamii, maktaba ya wanawake kupitia idara ya kusaidia usomaji katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha program chini ya anuani isemayo: (Jufunze usiyo yajua), inayo tokana na ratiba ya marafiki wa maktaba inayo lenga kukuza utamaduni wa kusoma vitabu, hii ndio njia nzuri ya kupambana na changamoto ya kutosoma vitabu.
Ustadhat Asmaa Abaadi kiongozi wa maktaba ya wanawake na mkuu wa program ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tumeandaa program hii kwa ajili ya kunufaika na msimu wa likizo, tumechagua kitabu kimoja na kukiingiza katika shindano la kuandika muhtasari wake kwa njia tofauti, mfano kwa njia ya michoro, mashairi, makala, na kuandika muhtasari wa kawaida, kutokana na viwango tofauti vya elimu, tumechagua kitabu kiitwacho (Uzuri katika mtazamo wa kimada na kimaana) kilicho andikwa na Ustadh Hassan Jawadi, nacho ni miongoni mwa matoleo ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, tutakusanya mihtasari kupitia kamati ya wataalamu watakao ichuja inayo faa, pamoja na kuandaa zawadi za washindi watakao tangazwa majina yao katika kongamano la wadau wa utamaduni”.
Ustadhat Miyaau Mussawiy kutoka kitengo cha kusaidia usomaji amesema kua: “Hakika idara ya kudumisha harakati kama hizi, mwaka huu umekua tofauti na miaka ya nyuma kwa kuchagua kitabu kimoja badala ya kuwa na vitabu vingi, kisha kuwashindanisha wasomaji wa kitabu hicho katika kuandika muhtasari wake, na kila mmoja ataandika kwa namna anayo penda, jambo hili litasaidia kugundua vipaji vya wasomaji na uwezo wao, kisha tunaweza kuangalia namna ya kunufaika na vipaji vyao, kwani mihtasari itaandikwa kwa njia tofauti, kwa mfano: njia ya mashairi, michoro, makala au kisa…, jambo lingine ni kuwepo kwa washiriki wenye umri tofauti na viwango vya elimu tofauti”.
Kumbuka kua maktaba ya wanawake imesha fanya program nyingi za aina tofauti ikiwemo program ya marafiki wa maktaba, nayo ni program inayo shajihisha usomaji wa vitabu, na kuongeza kiwango cha wasichana wanao jisomea dini yao jambo linalo saidia kuongeza uwelewa katika jamii.