Hazina ya nakala kale za Atabatu Abbasiyya tukufu.. ni ushahidi wa kimazingira na maarifa makubwa

Maoni katika picha
Nakala kale zinaumuhimu mkubwa katika uhai wa umma, ni chombo kilicho tutunzia elimu, maarifa, ufundi, adabu na habari za kihistoria na matukio yake, na matokeo yote ya kiakili, zina nafasi kubwa katika mawasiliano ya kimazingira kwenye umma, na kua sababu ya maendelea katika kila zama. Pia zina athari kubwa katika maendeleo ya mwanaadamu, pamoja na uhalisia wake wa kimaandishi, kuandikwa katika karatasi au ngozi na vifaa vingine vilivyo tumiwa na watu wa zamani katika uandishi, nakala kale ni miongoni mwa athari za kale zilizopo katika jamii ya kiislamu.

Dokta Usama Nakshibandi anasema katika makala yake iliyo andikwa katika jarida la turathi za Kairo: (watu wa kigeni wametambua umuhimu wa nakala kale katika uhai wa umma kwenye sekta zake zote, wakazilenga nakala kale kwa kuzishambulia na kuziiba katika vita walizo pigana, miongoni mwa wizi ujulikanao zaidi ni ule walioiba zaidi ya nakala kale (1200) katika nchi ya Iraq na wakazihamishia katika maktaba ya makumbusho nchini Uingereza, wizi huo ulifanywa na msafara wa mwingereza aliye andika safari yake na akamalizia kwa kuandika orodha ya nakala kale alizo ziiba na kuzipeleka Uingereza na kuziweka katika makumbusho ya Uingereza, akataja idadi yake katika makumbusho hiyo. Ripoti hiyo ilitolewa katika miaka ya themanini, akithibitisha nakala alizochukua katika maktaba ya makumbusho ya Iraq, ndipo kamati kuu ya turathi ikadai irudishiwe nakala kale hizo kwa kutumia ushahidi huo bila mafanikio, shirika la India mashariki lilinunua nakala kale zilizo kusanywa na bwana (Richadi Jonson) na kuzipeleka katika maktaba ya makumbusho ya Uingereza, nakala hizo zikawa sehemu kubwa ya maktaba hiyo, pia raia wa Swiden bwana “Martin” mwishoni mwa karne ya kumi na tisa alichukua nakala kale nyingi na baadhi yake akazipeleka Marekani, mwanzoni mwa karne ya ishirini masoko yakajaa nakala kale na turathi nyingi za Iraq, mwaka wa 1992m wakafanya maonyesho ya nakala kale hizo katika mji wa Paris, na mwaka 1910m walifanya maonyesho katika mji wa Mionikh, wakafanya tena Paris mwaka 1912m na mengine mengi yakaendelea kufanywa.

Miongoni mwa hazina kubwa zilizopo katika zama hini ni hazina ya nakala kale ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ilianzishwa mwaka 1382h, walijitahidi kukusanya vitabu muhimu elfu tano, zikiwemo nakala kale zipatazo elfu moja, nakala vizo za maandishi zilipatikana kutoka kwa watawala wa Ba’ath walio zikwa.

Pia vitabu vingi vilipatikana kwao, vilikua vimesha anza kuharibika, vitabu vingine walivitumia kama kuni za kupikia chai wanajeshi walipo teka Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya maandamano matukufu ya Sha’abaniyya mwaka 1411h.

Katika historia ya harakati ya kielimu ya Karbala inayo elezea hazina ya nakala kale za Atabatu Abbasiyya katika karne iliyo pita: (hazina hiyo ilikua na nakala kale 109 zenye umuhimu mkubwa na za zamani zaidi, ikiwemo misahafu ya zamani na nadra sana, mwanahistoria bwana Naasir Nakshabandi ametaja misahafu mitatu ukiwemo ulioandikwa kwa hati ya Kufiy, akasema ni misahafu ya kihistoria, hazina ya Atabatu Abbasiyya pamoja na hazina ya Atabatu Husseiniyya hazikusalimika na kuibiwa pamoja na kuporwa katika zama tofauti, kwani hazina hizo zilikua na vitu vya thamani sana, vilivyo wafanya wavamizi waliovunja heshima ya Karbala tukufu waibe vitu hivyo vya thamani.

Habari hizi zimetajwa katika kitabu cha Tarajidiyya Karbala kilicho andikwa na Haidari, anasema: (Katika Raudhwa ya Abbasi kuna hazina yenye vifaa na vitu vya thamani sana), wakati huo katika hazina ya Raudhwa kulikua na msahafu ulioandikwa kwa hati ya Kufiy iliyotiwa dhahabu, kulikua na misahafu mingine mikubwa inakadiriwa ilikua kumi na sita, pia kulikua na misahafu miwili midogo iliyo andikwa kwa hati ya Kufiy.

Mwenyezi Mungu amejaalia hazina hii tukufu ipate uhai upya, iendelee kuangazia utamaduni na maarifa, na iendelee kua kielelezo cha matendo mapya kwa ajili ya kesho ing’aayo.

Miongoni mwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu mtukufu imeandaliwa maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kufunguliwa upya baada ya kuangushwa kwa utawala wa kidikteta uliopita, na vifaa vyake vimerekebishwa kwa namna ambayo vinaendana na maendeleo ya zama hizi ya kielimu na kitamaduni katika taifa letu kipenzi, baada ya safari hii kupitia matatizo makubwa katika miaka ya mateso, katika miaka hiyo giza lilitanda kila sehemu, utamaduni haukuheshimiwa na sauti zilinyamazishwa.

Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu hazina hii imefunguliwa ikiwa katika muonekano mpya, ikimtegemea Mwenyezi Mungu mtukufu na baraka za Abulfadhil Abbasi mtoto wa kiongozi wa waumini (a.s).

Chini ya msaada mkubwa kutoka kwa Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Imamu Sayyid Sistani (d.dh) anamchango mkubwa katika kuhuisha maktaba za Ataba tukufu, maktaba zimepewa maelfu ya vitabu, na zimepangwa idara mpya, kama vile maktaba ya kielektronik, faharasi, uhakiki na uchapaji.

Chini ya miaka mitatu tangu kuhuishwa kwake yamepatikana maendeleo makubwa, idara kadhaa muhimu zimeanza kazi, kama vile idara ya kurepea nakala kale, upigaji picha nakala kale na faharasi na idara ya utunzi na utafiti, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu imekamilika na inaendana na mazingira halisi ya sasa, inakidhi mahitaji ya watafiti na wasomi tofauti.

Leo hii katika hazina ya Raudhwa ya Abbasi kuna maelfu ya nakala kale kama tunavyo ambiwa na Sayyid Nuriy Mussawiy mkuu wa Daru Makhtutwaat: “Juhudi kubwa zilizo fanywa zimezaa matunda ya kupatikana karibu nakala kale elfu tano katika hazina ya maktaba ya Ataba tukufu, ambazo ni miongoni mwa nakala kale muhimu sana, pia tumepata karibu nakala kale za picha laki moja na elfu hamsini kupitia ushirikiano na kubadilishana na maktaba na vituo vingine vya nakala kale.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: