Maahadi ya Qur’ani tukufu kupitia matawi yake yaliyo enea katika mikoa ya Iraq ina nafasi kubwa katika sekta ya Qur’ani, kwa ajili ya kuonyesha mafanikio yaliyo fanywa na matawi ya Maahadi na kubainisha mkakati wake ujao, tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Baabil limeandaa kongamano la Qur’ani kwa wanawake, linalo fanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha kiislamu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya chuo hicho, pamoja na ugeni rasmi unao wakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu na wanafunzi wa Maahadi.
Kongamano limekua na vipengele vingi, kikiwemo kipengele cha kuonyesha harakati za tawi hilo na Maahadi, kama vile semina za Qur’ani (hukumu za Qur’ani na tajwidi) zinazo tolewa katika maeneo yote ya mkoa wa Baabil, pamoja na semina za kuhifadhi chini ya ratiba makini iliyo andaliwa na idara ya Maahadi, pia kuna mradi wa beji la Qur’ani au mradi kamili wa masomo, unao husisha somo la tafsiri ya Qur’ani, hukumu za usomaji wa Qur’ani, Maarifa ya Qur’ani na masomo ya lugha ya kiarabu, pamoja na kufanya semina za majira ya joto na kushiriki katika vikao vya usomaji wa Qur’ani, na vituo vya kurekebisha usomaji wa Qur’ani kwa mazuwaru katika kipindi cha ziara ya Arubaini na zingine nyingi miongoni mwa harakati zinaho husu Qur’ani.
Kongamano limepambwa na maonyesho ya filamu na picha za semina mbalimbali zilizo fanywa na tawi la Maahadi mwaka jana, na wakaelezea mkakati wa Maahadi wa mwaka 2019m ambao utakua ni mwendelezo wa yale yaliyo fanywa mwaka jana, pamoja na kuongeza juhudi kwa ajili ya kuendeleza mazuri yaliyo pangwa na Atabatu Abbasiyya yukufu.