Ugeni kutoka maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya na wizara ya utamaduni na utalii ya Iraq wanatafunta njia ya kuongeza ushirikiano ya shirika la Unesco, katika sekta ya ukarabati wa nakala kale (makhtutwaat) na vifaa vingine pamoja na turathi zote kwa ujumla.
Hayo yametokea katika ziara waliyo fanya wizarani, na kukutana na afisa mahusiano wa wizara ya utamaduni na utalii bwana Falahu Hassan Shaakir Al’aniy, ambaye amefurahishwa sana kwa ziara hiyo, akaonyesha utayari wa wizara kufanya kazi pamoja na maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa faida ya Iraq, na kubainisha turathi ilizo nazo pamoja na kufikisha sauti hiyo kwenye shirika la Unesco, akasisitiza kua wizara iko tayali kusaidia mambo kama hayo.
Ustadh Liith Ali ambaye ni kiongozi wa kituo cha kurepea nakala kale amesema kua: “Katika ziara hii tumejadili namna ya kuwasiliana kati ya kituo cha kurepea nakala kale na shirika la Unesco katika sekta ya kurepea nakala kale pamoja na turathi zingine kwa ujumla, tumeelezea kwa ufupi ufanyaji kazi wa kituo na namna kinavyo repea nakala kale, naye Ustadh Ammaar Hussein kutoka maktaba ya kielektronik akatoa maelezo ya utendaji wa vituo vingine ambavyo viko chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na namna ya kunufaika na huduma zinazo tolewa na maktaba kwa lengo la kujiunga na shirika la Unesco, ukizingatia kua maktaba inaaminiwa na Unesco”.