Kituo cha turathi za Karbala kinabainisha nafasi ya Marjaiyya katika kujenga taifa la Iraq...

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kwa kutumia vitu tofauti, kimekua kikiandaa mada zenye madhumuni na fikra za kuunganisha matukio yaliyo pita na ya sasa, na kuziwasilisha kupitia nadwa, makongamano au machapisho (vitabu), chapisho lake la mwisho linaitwa (Nafasi ya Marjaiyya katika kujenga taifa la Iraq).

Nalo ni miongoni mwa mfululizo wa machapisha ya kituo cha turathi, ndani ya chapisho hili kuna misimamo, mitazamo na fatwa za Aayatullahi Shekh Muhammad Taqi Shirazi (q.s) na Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Aayatullahi Sayyid Sistani (d.dh), kimeandikwa na Dokta Imaad Kaadhwimiy, kitabu hicho kina sehemu mbili, sehemu ya kwanza inaelezea fatwa ya jihadi katika mapambano ya Ishirini na mchango wake katika kuasisiwa taifa la Iraq, na sehemu ya pili inaelezea fatwa ya jihadi ya kifaya iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ali Sistani (d.dh) na nafasi yake katika kulinda taifa la Iraq na umoja wake.

Kumbuka kua kituo cha turathi za Karbala kinaendelea kuandika vitabu na majarida pamoja na orodha za turathi za mji wa Karbala kutokana na utafiti na uhakiki wanao fanya, na kuhakikisha tunazipatia maktaba za kiarabu na kiislamu machapisho bora, sambamba na kuangazia nafasi ya pekee ya mji wa Karbala kwenye sekta zote za elimu na maarifa.

Kwa anaye hitaji kuona kitabu hiki pamoja na vitabu vingine atembelee maonyesho ya vitabu ya kudumu yaliyopo karibu na mlango wa Kibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: