Program ya hema la fatwa ya ushindi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu imeanza

Maoni katika picha
Baada ya mafanikio yaliyo patikana katika awamu ya kwanza ya hema la skaut ya wanafunzi wa vyuo vikuu, leo idara ya mahusiano na vyuo vikuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, inafanya program mpya iliyo pewa jina la (hema la fatwa ya ushindi la skaut), kama sehemu ya kuenzi ushindi wa raia wa Iraq dhidi ya magaidi wa Daesh, na kufanikiwa kwao kukomboa ardhi yote ya Iraq iliyo kua imetekwa na magaidi hao, katika program hii wanashiriki zaidi ya wanafunzi (60) wa vyuo vikuu, katika eneo la Kasaarah ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu karibu na ngome ya Akhidhwar kwenye jangwa la Karbala tukufu.

Ustadh Maahir Khalidi Almiyahi kiongozi wa harakati za vyuo vikuu, ameongea na sisi kuhusu hema hilo kua: “Tumeweka hema kwa ajili ya kutoa muongozo wa kitamaduni, kimalezi pamoja na mambo mengine mbalimbali, ili kunufaika na kipindi cha likizo na kuhakikisha kinatumika vizuri”.

Akaongeza kua: “Hema litadumu siku nne na litakua na vipengele vifuatavyo:

  • - Mihadhara ya fiqhi, aqida na maelekezo ya kimalezi inayo tolewa kulingana na umri wao pamoja na viwango vyao vya elimu, mihadhara inayogusa maisha yao kielimu, kikazi na katika mazingira ya nyumbani.
  • - Mashindano ya kidini, kielimu, kitamaduni, kihistoria, kijografia na kilugha.
  • - Masomo na mihadhara ya maendeleo ya binaadamu inayo saidia kukuza uwezo wao.
  • - Vikao vya mijadala kuhusu hali ya taifa kwa ujumla.
  • - Vipindi vya mapumziko (kubarizi).
  • - Kutembelea sehemu mbalimbali.
  • - Mashindano ya michezo”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu husimamia na kuendesha program mbalimbali za kielimu na kitamaduni ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya tukufu zinazo lenga wanafunzi, kwa ajili ya kujenga misingi imara ya mafundisho ya Dini tukufu ya kiislamu kwa mujibu wa mwenendo wa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) sambamba na kujenga uzalendo wa kitaifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: