- - Kaswida na mashairi yanayo elezea dhulma alizo fanyiwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s).
- - Kuelezea hatua mbalimbali kihistoria ilizopitia madhehebu ya Ahlulbait (a.s) kwa kulinganisha na zingine.
- - Kuweka mazingatio katika jambo moja au nukta moja ya kila hatua ambayo lilitokea badiliko katika madhehebu ya Ahlulbait (a.s).
- - Jeduali kuhusu Uimamu na majaribio ya kuuzima yaliyo fanywa na baadhi ya watu wa zama za mwanzo kwa kuwanyanyasa wafuasi wa Ahlulbait (a.s).
- - Majibu yaliyo tolewa na wanachuoni ambao ni wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kwa waliotaka kutweza Uimamu na kuidharau madhehebu ya Ahlulbait (a.s) sambamba na kuongelea dhulma alizo fanyiwa bibi Zaharaa (a.s).
- - Kuangalia yaliyo andikwa dhidi ya madhehebu ya Ahlulbait (a.s) katika zama za hivi karibuni, pamoja na kuangalia majibu yaliyo tolewa na wanachuoni wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbait (a.s), wametunga vitabu vingi vinavyo jibu kila swala walilo tuhumiwa.
- - Utukufu wa Bibi Zaharaa (a.s) mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).
- - Kuangalia uhusiano kati ya bibi Zaharaa (a.s) na wafuasi wake”.
Muhani akamaliza kwa kusema: “Hakika ni vigumu sana kuzungumzia utukufu wa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya baba yake Mtume (s.a.w.w), ni sahihi kusema: Hakika yuko juu ya uwezo wa kalamu na ulimi katika kumuelezea, kwa ajili ya kuchota japo kidogo katika bahari hii kubwa isiyo kauka tunatoa mihadhara hii kwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na mazuwaru watukufu”.