Shule za Alkafeel za wanawake zimezindua hema la mafunzo ya kiutamaduni kwa wanafunzi wa vyuo vikuu…

Maoni katika picha
Kutokana na kuingia kipindi cha likizo, shule za Alkafeel za wasichana katika kituo cha Swidiiqah Twaahirah (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, zimezindua hema la utowaji wa mafunzo maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu, hema hizo nimepata wanafunzi wapatao (172) watakao shiriki mafunzo hayo, mafunzo yatadumu kwa muda wa siku tano, kunakua na program mbalimbali, mada watakazo fundishwa zinalenga kuwajenga kifikra na kuwafanya waweze kupambana na changamoto za kidini, kitamaduni na kijamii, kiongozi wa shule za Alkafeel za wanawake Ustadhat Bushra Kinani ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu program ya hema hizo kua: “Hema hizi ni mwendelezo wa harakati tulizo kua tukifanya kwa ajili ya kunufaika na kipindi cha likizo kwa kuwajenga kiutamaduni na kutambua utukufu wa mwanafunzi”.

Akaongeza kua: “Hema hizi zimeandaliwa kwa kushirikiana na kituo cha utamaduni wa familia, na kufadhiliwa na kitengo cha Tarbiyya na Taaliim cha Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na idara ya maktaba ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ili tuweza kutumia kila fursa inayo patikana kwa kuwajenga wanafunzi wetu, na kujenga misingi imara katika jamii, kutakua na mafunzo tofauti kwenye hema hizo za skaut, kwa kutumia ratiba makini inayo endana na washiriki pamoja na kutofautiana viwango vyao”.

Akamaliza kwa kusema: “Hema hizi zinaupekee wake, zimeandaliwa kwa ajili ya kipindi cha likizo na zitadumu siku tano (5), wanafunzi washiriki ni (172), hii ni dalili ya mafanikio, wanafunzi hao wanatoka kwenye vyuo vikuu vya mkoa wa Waast na Karbala tukufu”.

Kumbuka kua hema hizi ni sehemu ya harakati zinazo fanywa na idara ya shule za Alkafeel za Qur’ani, na kufanyika ndani ya kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s), ratiba ya mada watakazo fundishwa inaweza kuendelea kutumika mwaka mzima, kutakuwa na warsha ya kielimu katika sekta tofauti kwa ajili ya kukuza uwezo wao wa kielimu na kijamii, sambamba na kuwapa mihadhara mingi kuhusu kufanya kazi ya kubadilisha mtazamo wa jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: