Kiongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu aipongeza kamati yake mpya na awasifu wajumbe wa kamati hiyo waliotangulia…

Maoni katika picha
Katika kikao kilicho husisha kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Ataba tukufu, kikiwa kikao cha kwanza cha kamati hiyo mpya, Sayyid Swafi amewashukuru wajumbe wa kamati iliyo pita kwa kazi nzuri walizo fanya wakati wa uongozi wao.

Na akatoa pongezi kwa wajumbe wa kamati kuu mpya iliyo anza kazi karibuni, pamoja na katibu mkuu wake Mhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) ambaye ameongezewa muda wa uongozi kwa miaka mitatu ijayo na msaidizi wake mpya Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi.

Sayyid Ahmadi Swafi amewasisitiza wajumbe wapya kufanya kazi kwa bidii na kuendeleza mazuri yaliyo anzishwa na viongozi waliomaliza muda wao katika kuwahudumia mazuwaru wa malalo tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mheshimiwa akasifu mambo yaliyofanywa na kamati kuu iliyo pita kwa utumishi mzuri waliokua nao katika malalo tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika kipindi chote walichokua madarakani.

Fahamu kua kamati mpya inawajumbe wafuatao:

  • - Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi (katibu mkuu msaidizi).
  • - Mheshimiwa Sayyid Liith Najmu Abdullahi Mussawiy.
  • - Dokta Abbasi Wahabi Didah.
  • - Ustadh Jawadi Kaadhim Hasanawiy.
  • - Ustadh Kaadhim Abdulhussein Ubaadah.
  • - Sayyid Mustwafa Aali Dhwiyaau-Dini.

Kumbuka kua Ataba na mazaru za Iraq zipo chini ya kanuni ya 19 ya mwaka 2005m iliyo tungwa na mamlaka ya kwanza ya kisheria iliyo chaguliwa, ambayo imeziweka chini ya uongozi wa Waqfu Shia ambao upo chini ya serikali ya Iraq, kifungu cha nne (4) kikatoa sharti kua Marjaa Dini mkuu ndio mwenye haki ya kumpasisha kiongozi mkuu wa kila Ataba kabla ya kuteuliwa na uongozi wa Wakfu Shia, ndipo Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani (d.dh) tarehe (19 Rabiul Awwal 1437h) sawa na (31/12/2015m) akatoa hati ya maandishi ya kumpasisha wakili wake Allaamah Hujjah Sayyid Ahmadi Swafi kua kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: