Mwendelezo wa nadwa zake: Maahadi ya turathi za mitume na chuo kikuu cha Ummul Banina zinafanya nadwa (darasa mjadala) kwa wanafunzi wake

Maoni katika picha
Maahadi ya turathi za mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa wavulana na chuo kikuu cha Ummul Banina (a.s) cha masomo ya masafa kwa wasichana, chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu zimefanya nadwa (darasa mjadala) kwa wanafunzi wake wa mkoa wa Bagdad.

Nadwa hiyo imehudhuriwa na idadi kubwa ya wanafunzi wa Maahadi na chuo kikuu, imefanywa kwa mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mji mtukufu wa Kadhimiyya na kuhudhuriwa na mwakilishi wa Marjaa huyo wa mkoa wa Bagdad mheshimiwa Shekh Hussein Aali Yasini, ambaye alitoa neno katika nadwa hiyo, akazungumzia furaha yake na kuridhishwa kwake na jambo hili, pamoja na hatua iliyo chukuliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kutoa elimu ya Dini kwa kutumia teknolojia za kisasa, na kuhakikisha wananufaika na teknolojia hiyo na akahimiza kila anaye penda kusoma ajiunge na masomo hayo, akasifu jambo hilo na namna linavyo saidia kupata elimu katika zama zetu, akaongeza kusema kua: “Hakika jukumu la kutafuta elimu sahihi ya Dini kwa vijana lipo mikononi mwa wazazi na kwa kijana mwenyewe”, akasisitiza kua: “Hakika kusoma kielektronik ni mapinduzi mapya ya njia za usomaji, na maendeleo mazuri katika sekta ya elimu”.

Pia kulikua na ujumbe wa mkuu wa Maahadi ya turathi za mitume (a.s) ya masomo ya hauza ya kielektonik ambaye alisema kua: “Hakika usomeshaji wa njia ya masafa ni jambo zuri linalo fanywa chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, tutakua tunafanya nadwa za wanafunzi wa Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) na wa chuo kikuu cha Ummul Banina (a.s) cha kuandaa wahadhiri wa kike kwa ajili ya kudumisha ustadi wake, chini ya utaratibu uliopangwa wa kusikiliza maoni na ushauri wa wanafunzi na kutoa majibu ya maoni na fikra zao”.

Yametolewa maoni tofauti yanayo husu mwalimu na mwanafunzi pamoja na changamoto na namna ya kuzitatua, sambamba na kujadili namna ya kuboresha masomo, pamoja na kutolewa maelezo ya mitandao iliyo chini yao.

Kumbuka kua miongoni mwa mambo yanayo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni na yaliyo onyesha mafanikio ni masomo kwa njia ya masafa, kupitia Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) na chuo kikuu cha Ummul Banina (a.s), tunafanya nadwa za kielimu kila baada ya muda fulani na kujadili changamoto pamoja na namna ya kuzitatua ili kudumisha mafanikio haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: