Imetokea hivi punde: Faharasi ya nakala kale zilizo hifadhiwa katika maktaba maalumu za Karbala…

Maoni katika picha
Imetokea hivi punde katika kituo cha kupiga picha nakala kale na faharasi chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa matolea yake ni (Faharasi ya nakala kale zilizo hifadhiwa katika maktaba maalum za Karbala), limefanyika hili kwa ajili ya kuangazia maktaba maalum zilizopo katika mji mtukufu wa Karbala, ambazo ni urithi mkubwa na mwalimu muhimu wa mambo ya Dini.

Kwa mujibu wa maelezo ya kituo toleo (kitabu) hicho kina faharasi ya nakala kale kutoka katika maktaba tofauti za mji mtukufu wa Karbala, miongoni mwa maktaba hizo ni: (Maktaba ya Shamsu Fuqahaau, maktaba ya Sayyid Kaadhim Naqibu, Maktaba ya Sayyid Salmaan Haadi Aali Twa’amah, maktaba ya Shekh Abduridhwa Swafi, maktaba ya Shekh Muhammad Ali Daa’il-Haqi, maktaba ya Sayyid Gharifi, maktaba ya Shekh Haadi Khafaaji Karbalai, maktaba ya Ustadh Abdurasuul Khafaji, maktaba ya Rasulul-A’adham na maktaba ya Dokta Hamidi Majidi Hadu).

Kituo kikabainisha kua idadi ya nakala zilizo tambuliwa katika kitabu hiki zimefika mijaladi (159) zikiwa na anuani (majina) mia moja sabini (170) pia kuna nakala muhimu bado hazija hakikiwa hadi sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: