Wahudumu wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu ni mikono isiyojua kuchoka…

Maoni katika picha
Wahudumu wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika watumishi wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya kupitia idara tofauti, miongoni mwa idara hizo ni idara ya utumishi, ambayo inafanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya kuhakikisha uwanja wa katikati ya haram mbili unakua katika muonekano mzuri.

Mtandao wa kimataifa Alkafeel umezungumza na kiongozi wa idara ya utumishi katika kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu Maliki Khaliil Janabi ambae amesema kua: “Ukubwa wa eneo letu la kazi unaanzia mlango wa Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) katika Atabatu Abbasiyya hadi mlango wa kichwa kitukufu katika Atabatu Husseiniyya tukufu kwa kupitia uwanja wa katikati ya haram mbili, pamoja na barabara zinazo zunguka uwanja huo”.

Akaongeza kua: “Idara hii inakazi nyingi, kuna kazi za kusafisha barabara zinazo zunguka uwanja wa katikati ya haram mbili, upigaji deki wa barabara kwa kutumia gari maalumu zinazo milikiwa na idara hiyo ni ratiba ya kila wiki, pamoja na kusafisha eneo la marumaru la wazi au sehemu zenye paa, deki hupigwa baada ya kutandua mazulia yaliyo tandikwa katika eneo hilo kwa ajili ya swala au kupumzika, kazi hiyo hukamilika kwa siku mbili, deki hupigwa kila wiki”.

Akaendelea kusema: “Tunasafisha pia madeli ya maji ya kunywa na sehemu za kutawadhia pamoja na uzio wa chuma, kazi haiishii hapo, bali tunadumisha usafi katika uwanja huo na barabara zinazo uzunguka saa ishirini na nne (24), hadi wanapokaa mazuwaru, tunawatumishi wapatao (120) wanazamu tatu, (asubuhi, jioni na usiku)”.

Kuhusu kazi ya kupiga deki amesema kua: “Mchana wa kila Jumapili na Jumatatu huwa tunapiga deki katika maeneo yaliyo pauliwa ndani ya uwanja wa eneo ka katikati ya haram mbili tukufu, na usiku huwa tunapiga deki barabara, kutokana na uchache wa msongamano wa mazuwaru usiku wa siku mbili hizo, hufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na ndugu zetu watumishi wa idara ya mitambo (magari) ambao huchukua jukumu la kuandaa gari maaluzu za maji kwa ajili ya deki, siku ya Jumanne na Jumatano huwa tunasafisha vitu vilivyopo katika uwanja na barabara zinazo zunguka uwanja huu, kuhusu upigaji wa deki eneo la katikati ya ndani ya uwanja wa haram mbili tukufu, eneo hilo hupigwa deki kila baada ya siku (14) na mara nyingi husadifu siku ya Ijumaa”.

Akasema kua: “Kila mwezi idara yetu husafisha njia za maji zinazo zunguka eneo la katikati ya haram mbili tukufu, kwa kutumia gari maalum kutoka idara ya magari au idara ya mkoa mtukufu wa Karbala, tumeamua kufanya hivyo kwa sababu ya njia hizo kuziba katika siku za mvua nyingi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: